Ghost aisifia Patanisho na Gidi. Asema kinachofanya shoo hii ipendwe zaidi

67572951_122315605801944_5858248206995081202_n
67572951_122315605801944_5858248206995081202_n
Ghost Mulee ametoa sifa zote za mtangazaji mwenza Gidi zinazofanya shoo ya Patanisho kuwa moto wa kuotea mbali.

Kipindi hiki sasa kimepigiwa upatu mkubwa kwa kura bora zaidi nchini.

Soma hadithi nyingine:

Ghost ni mtangazaji katika kituo cha Jambo katika kipindi kinachoruka kila asubuhi.

Akizungumza katika mahojiano leo, kocha huyu wa soka alianza kwa kusimulia umuhimu wa shoo hii,

"Nahisi kwamba Patanisho inagusa maisha ya kawaida katika ndoa zetu kwanza. Nimeingia katika mambo ya utangazaji kiajali au labda destiny."

"Patanisho ni ya ukweli. Ndugu wanapokosana tunawaleta pamoja . Ni kioo cha jamii katika maswala ya ndoa."

Soma hadithi nyingine:

Ghost amesema kuwa hakuna shule ya ndoa ya kujifunza kwa hivyo watu ujifunza mengi kutoka kwa visa mbalimbali vya wenzao.

Ghost amesema kwamba kipindi hiki kinahitaji mtu kama Gidi,

"Gidi ni mkakamavu. Ana ushauri mzuri na wasia. Ana uwezo wa kudadisi anachotaka msikilizaji na kumjibu sawa."

Huku akiongoza kuwa Gidi hujitahidi sana kutojawa na hasira katika mawasiliano ya simu,

"Kuna watu wanachukua muda sana kueleza kisa chao kwa dakika chache ila yeye huwavumilia."

Soma hadithi nyingine:

Baada ya studio, Ghost amesema yeye hujipa raha katika uraibu wa kutembelea mbuga za wanyama.

"Napenda wanyama sana na misitu. Binadamu wamenichosha wengi ni waongo. Nikiona simba akiua nafurahi zaidi. Nikisikiliza muziki nafurahi zaidi."