Ghost Mulee amshauri Victor Wanyama kabla ya kipute cha AFCON

Ghost.Mulee.and.Wanyama
Ghost.Mulee.and.Wanyama
Kipute cha ubingwa bara Afrika, AFCON kinang’oa nanga hii leo huku wenyeji misri wakikabana koo na Zimbabwe.

Misri al maarufu the pharaohs, wakiongozwa na mshambulizi matata wa Liverpoool, Mo Salah wana rekodi ya mataji saba na watakuwa wananuia kuongeza la nane baada ya kunyukwa katika fainali ya mwaka 2017 na Cameroon.

Mara ya mwisho Kenya ilishiriki katika michuano ya AFCON ilikuwa miaka kumi na mitano iliyopita, chini ya uongozi wake kocha Jacob 'Ghost' Mulee.

Kocha huyo ambaye sasa ni mtangazaji wetu, ana imani kuwa vijana wa Harambee Stars wataleta hadhi kuu nchini na kuwa watafuzu hadi raundi ya mchujo.

Kenya iko katika kundi 'C' na Algeria, Tanzania na pia Senegal.

Baada ya Wanyama kufuzu kwa fainali za kombe la mabingwa bara uropa dhidi ya Liverpool, Mulee alimshauri nahodha huyo kuwa anapaswa kuuleta msukumu huo huo kwa timu ya taifa.

Soma ushauri wake,

Kwanza nampongeza Victor Wanyama kwa kusaidia Tottenham kufuzu hadi fainali za kombe la mabingwa bara uropa. Kama nahodha ameongoza kwa mfano na hakuna tuzo kuu kwa mchezaji kama kucheza katika kombe la dunia na pia katika fainali za kombe la mabingwa bara uropa.

Huo ushawishi, huo msukumo na maadili mema twaomba ulete katika timu ya taifa katika kombe la ubingwa bara Afrika.

Watu wengi wasema kuwa ndoto ya Kenya tayari imedidimia lakini mimi naamini kuwa tutaizaba Algeria kisha tutoke sare na Tanzania katika mechi ngumu, na pointi nne zitakuwa tosha kutupeleka katika raundi ya mchujo.

?t=84