Ghost na Arocho wapanga kukuza vijana kupitia kadanda

soccer agents L to R Patrick Murk from Sweden, Jamal Ibrahim, Fred Arocho and Johan Sandohl from Sweden at the Odibets Champions tournament
soccer agents L to R Patrick Murk from Sweden, Jamal Ibrahim, Fred Arocho and Johan Sandohl from Sweden at the Odibets Champions tournament
Watangazaji wa Radio Jambo, Fred Arocho na Jacob 'Ghost' Mulee ni miongoni mwa watangazaji ambao taaluma zao za uanahabari zimejengwa kwa msingi wa kadanda.

Kwa mfano, Afrika mzima, yajua kuwa Ghost Mulee ni mmoja wa makocha maahiri na humu nchini anatambulika kama gwiji kwa ujuzi na mafanikio aliyoletea nchi hii.

Arocho ama ukipenda 'Twiga' pia anaheshimika nchini kwa mchango wake kama mchezaji, enzi zile na hata pia ndani na nje ya uwanja na studioni, ambapo anatetea maswala ya wachezaji.

Pamoja, wawili hao wameshirikiana ili kukuza talanta na isitoshe, ni mpango wao kuonesha fahari yao kwa Nairobi na haswa Eastlands, mtaa ambao walilelewa.

Moja wapo ya mipango wao ni kuandaa shindano la kadanda la wachezaji 11 kila upande, shindano ambalo litaleta pamoja timu nane kutoka mitaa tofauti ya Nairobi.

Shindano hili ambalo limedhaminiwa na OdiBets, ni la siku moja, linafanyika hii leo katika uga wa Camp Toyoyo, Jericho.

Isitoshe, wawili hao wameshirikiana na ajenti kadhaa kutoka Sweden wakiwemo; Patrick Murk na Johan Sandohl na pia Jamal Ibrahim, ambao watakuwa wakitafuta talanta ambazo watakuza.

"Ghost Mulee nami tulileta vichwa vyetu pamoja kama watu walioanzia Eastlands, watu ambao walipata fursa ya kucheza kadanda na kufika tulipo. Sasa tunataka kupatia wengine fursa kama ile ili wajikuze." Alisema Arocho.

Aliongeza,

Tumechukua timu nane kutoka Nairobi kote ambazo ndio timu bora kabisa Nairobi ili waoneshe talanta zao. Na wakibahatika watajipata bara Uropa. Shindano lile litaanzia robo fainali, kisha nusu fainali hadi fainali."

Shindano hilo liitwalo 'Champions of champions' tayari limeanza na litakamilika saa kumi na moja jioni.

Washindi watazawadiwa kitita cha elfu 50,000 huku watakaopoteza katika fainali watapokea elfu 20,000.