Gianni Infantino achaguliwa tena kuliongoza shirikisho la FIFA

 Gianni Infantino  amechaguliwa tena kuwa Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa  katika mkutano wa wanachama wa shirikisho hilo la soka ulimwengui jijini Paris .

Infatino mwenye umri wa miaka 49  aliyechukua usukani katika shirikisho hilo mwaka wa 2016  baada ya kuondoka kwa Sepp Blatter  hakupingwa  kwa muhula mwingine wa miaka mine hadi mwaka wa 2023 .

Awali ,Infantino  alisisitiza kwamba fifa limegeuzwa kuwa shirikisho linaloambatana na   vigezo vya kuaminika na hadhi  alipokuwa akiwahutubia wajumbe 211 wanachama wa shirikisho hilo .

" Leo hakuna anayezungumza kuhusu migogoro ,hakuna anayezungumza kuhusu kuijenga fifa kutoka chini wala sakata  za ufisadi,tunazungumza tu kuhusu soka’ amesema mkuu huyo wa fifa ambaye awali  alikuwa katibu mkuu wa shirikisho la UEFA .