Hatua hiyo huenda ikatafsiriwa kama kumpepeza Gideon katika kilele cha usemi katika jamii ya wakalenjin. Gideon na naibu wa rais William Ruto wamekuwa katika nipe nikupe ya kujaribu kuchukuwa uongozi wa jamii hiyo kisiasa lakini baada ya uchaguzi wa 2013 ambapo Ruto aliungana na Uhuru Kenyatta kuunda serikali ,amechukuliwa kama ‘kiongozi’ wa wakalenjin kisiasa . Wakati wa hafla fupi ya kumpa Gideon Rungu hiyo Raymond amesema –
‘KWA VILE MZEE ALITULINDA ,NA KULINDA KENYA VIZURI ,TUNAAMBIA HUYU(Gideon) KANU IAMKE.. NA TUKO NA BBI ,WE WANT TO BE PART OF IT..WE SUPPORT BBI’ amesema Raymond .
Alipoichukua rungu hiyo ,Gideon aliahidi kufanya kadri ya uwezo wake kufaulu katika jukumu lake la kuiongoza familia ya Moi kisiasa .
‘HATA KUSHIKA HII RUNGU…ANYWAY…NITAJARIBU ..NIKIWEKA MWENYEZI MUNGU MBELE,MENGI TUTASEMA BAADAYE’. Amesema Gideon .Kakake