Gidi afurahishwa na picha ya mwanawe akisoma Kitabu chake Lupita

sulwe (1)
sulwe (1)
Mkenya na muigizaji maarufu duniani, Lupita Nyong'o ambaye ni mwanawe gavana wa Kisumu, Anyang' Nyon'go anajulikana kwa ustadi wake kimitindo.

Hata hivyo mbali na hayo, anajulikana kwa kazi yake ya kuhamisisha umma kuhusu umuhimu wa kupendana bila ubaguzi wa rangi.

Hayo amefanya hadi kupitia kitabu chake kwa jina 'SULWE' ambapo anasimulia kisa cha mtoto wa kike ambaye ana rangi nyeusi na ambaye lengo lake kuu ni kuwa mweupe.

Hadithi hiyo inasimulia jinsi watu wanapaswa kujipenda jinsi walivyo umbwa na mwenyezi mungu.

Gidi kupitia mtandao wake wa Insta, alichapisha picha mwanawe Marie-Rose Ogidi, akisoma kitabu hicho cha Lupita huku akielezea kufarahishwa kwake.

Kulingana na mtangazaji huyo, mwanawe ambaye anaishi Ufaransa na mamake, yeye ndiye mwanafunzi pekee wa asili ya Afrika katika darasa lao.

Anasema kuwa ni ombi lake kuwa kitabu hicho cha SULWE kitamsaidia Marie-Rose kuelewa na kuikubali ngozi yake katika maisha mwake ya usoni.

Soma ujumbe wake,

Waking up to this photo of Marie-Rose going through her favourite book SULWE by 

Sulwe is a children's fiction picture book by actress Lupita Nyong'o. It follows the story of a young girl who wishes for her dark skin to be lighter. The story is ultimately about colorism and learning to love oneself, no matter one's skin tone

Marie-Rose is growing up in a multiracial environment where issues of color normally arises. She is actually the only black kid in her class. Although it doesnt bother her at this tender age, but I hope this book will build a foundation that will help her understand and appreciate her skin color in future

Thank you  for inspiring these angels at a tender age 🙏🙏