Gidi amkosoa rapa Khaligraph Jones

Rapa mkubwa Afrika mashariki Khaligraph Jones almaarufu kama Papa Jones ni kati ya wasanii wanaofanya muziki wa kuchana hapa nchini.

Mkali huyu wa nyimbo inayofanya vyema katika mitandao na katika vyombo vya habari ya Superman mapema mwakani alionekana kukerwa na kuona redio na runinga hazichezi nyimbo za wasanii hapa nchini na kuapa kuwapeleka nchini Nigeria ili wajifunze kutoka nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Soma hapa:

Katika mahojiano ya kipekee na kituo cha Jambo, Gidi amezungumzia maswala yanayogusia muziki wa hapa nchini na jinsi wasanii wanavyojituma katika tasnia hii.

Gidi ameonekana sana kumkosoa msanii huyu kwa kutofahamu utaalamu unaotumika katika redio na runinga.

“Khaligraph jones ni msanii mzuri. Lakini huenda kidogo hana ufahamu wa jinsi redio zinafanya kazi. Mtangazaji wa redio hana mamlaka ya kuchagua muziki gani anafaa aucheze. Kila redio ina mtindo inayofuatilia. Miziki tunayocheza redio Jambo huwezi kuicheza Classic Fm kwa sababu wasikilizaji wao wanataka vitu tofauti.”

Soma hapa;

 Huku akionekana kuwakashifu wasanii wanaofanya nyimbo kujulikana tu na kuwa na sifa bila kuzingatia kutengeneza hela, Gidi alisema kuwa wasanii nchini wanatakiwa waige mfano wa kundi la wasanii la Sauti Sol.

“Kila msanii anajitahidi sana. Sauti Sol naweza nikasema wanaufanya muziki kitaalam sana.Wasanii chini nawaomba sana waweze kuiga kikundi hiki.”

Soma hapa:

Gidi anawahimiza wasanii waache mtindo wa kuimba nyimbo kujulikana tu bali watengeneze pesa.

“Wafanye muziki kama biashara na sio kuufanya ujulikane na watu. Ni biashara. Ni kazi.”

Akiwalenga wasanii wanaoipa nguvu hashtegi ya #PlaykenyanMusic, mtangazaji huyu wa kipindi kinachoruka kupitia masafa ya Redio Jambo cha Patanisho, alidokeza kuwa redio nyingi hapa nchini ni biashara za watu binafsi.

"Tusije tukaanza kushurutisha nyimbo kuchezwa katika redio. Redio zingine ni biashara za watu binafsi. Labda serikali inaweza kuwa na sheria zinazohakikisha tunacheza miziki ya hapa nchini kwa kiwango kikubwa.”