Gidi Na Ghost Wapata Mialiko Ya Nyama Ya Mbuzi Na Papa Baada Ya Raila Kufanywa Kinara Wa NASA

Siku ya Alhamisi wakenya wote walitegea kwa hamu na ghamu ili wamfahamu ni nani kati ya viongozi wa upinzani, wakiwemo Raila Odinga, Stephen Kalonzo, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula atakaye peperusha bendera ya muungano wa NASA, ifikapo mwezi wa Agosti tarehe nane.

Vigogo hao wa kisiasa waliwaalika wafuasi wao kwa wingi katika bustani ya Uhuru huku wakiahidi kutaja kinara wao, baada ya siku nyingi za kujadiliana pia wakimaliza uvumi ambao ulikuwa umeenea kuhusu kutoelewana kwao.

Basi siku ilipotimia kiongozi wa ODM, Raila Odinga ndiye aliyetangazwa kuwa kiongozi atakaye wania kiti cha urais dhidi ya Rais Kenyatta huku Kalonzo Musyoka akiwa naibu wake, kama wengi walivyotarajia.

Nao Moses Wetangula, Musalia Mudavadi na Isaac Rutto wakiwa mawaziri ambao wataeneza utendakazi wa serikali hiyo iwapo wataibuka washindi.

Tangazo hilo lilibua hisia mbali mbali huku wengine wakifurahia uamuzi huo nao wengine wakidai kuwa haina tofauti yoyote na mwaka wa 2013 na kuwa wangempa kiongozi mwingine nafasi ya kuwania urais.

Basi wapenzi wa Radio Jambo waliwashangaza watangazaji, Gidi na Ghost walipowaalika katika sherehe zao za kusherehekea hatua ya NASA huku mmoja wao akiwaalika nyama ya mbuzi, huku mwingine akijitolea kuwanunulia nyama ya papa.

"Nakuambia bwana Gidi nimelala kwa kitanda nimetosheka. Mimi ni yule shabiki wa Raila, mimi ni mtu wa Raila tangia mwaka wa 2002." Alisema bwana Ngugi kutoka maeneo ya uwanja wa ndege wa Wilson. "Nataka utafute siku na Ghost mimi nakaa hapa Wilson unipigie simu ukuje tukule mbuzi." Aliongeza.

Baadaye bwana Peter Luta shabiki sugu wa Radio Jambo kutoka meneo ya Bombolulu Mombasa, aliwapa watangazaji hao mwaliko mwingine, akiomba awanunulie papa na mamba.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be