Hali imeonekana kuwa mbaya baada ya mbunge wa cherengany Joshua Kutuny kumshtumu Mi kwa kutojali maslahi ya watu wa Rift Valley .
Isitishe ,washirika wake wa karibu na wenye ushaiwishi katika chama chake mbunge wa Emurua Dikir Johana Ng’eno na gavana wa West Pokot John Lonyangapuo - wameonakana kuanza kuegemea upande wa naibu w arais William Ruto .
Ng’eno ametangaza hadharani kwamba atamuunga mkono DP Ruto kugombea urais mwaka wa 2022 . Kulingana naye toshi ya uongozi wa wakalenjin itaelekea Nandi mwaka wa 2022 kupitia Ruto kuisha ije kwa jamii ya Kipsigis
Gideon, ambaye ni seneta wa Baringo ni miongoni mwa viongozi wanalenga kumrithi rais Uhuru Kenyatta . Kutuny amesema alifiiri Gideon ni bora zaidi ya Ruto lakini amegeuka kuwa ‘mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo ‘
Mbunge huyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa DP Ruto na hatua yake ya kubadilisha msimamo huenda ikawa na athari katika kambi ya Gideon Moi . Ameliambia gazeti la the Star ;
“Gideon sasa ni adui ya watu wa Rift Valley .Anawatambua maafisa wakuu watendaji katika mashirika ya serikali kutoka Rift valley kisha kusababisha wafutwe kazi kwa madai kwamba ni washirika wa DP Ruto’
Kutuny ndiye sura ya mrengo wa kielweke katika eneo la Rift valley . tatizo lake la Gideon limetokana na mageuzi yaliofanywa katika shirika la KURA
Wote walikuwa wamekubaliana kwamba Luka Kimeli ambayealikuwa maneja mkurugenzi wa Kyura na mkaazi wa cherangany athibitishe kama mkurugenzi mkuuu wa maamlaka hiyo
Ha hivyo ,kulingana na Kutuny ,Gideon alikiuka makubaliano hayo yaliyokuwa yameidhinishwa na rais Kenyatta na kushawishi uteuzi wa Philemon Kandie katika nafasi hiyo.Kandie anatoka Baringo