Gloves are Off! Ruto apuuza BBI ya Raila na Uhuru

RUTO 2
RUTO 2
Naibu wa rais  William Ruto   ametuma ujumbe katika twitter unaoonekana kupiga vijembe juhudi za  Kiongozi wa ODM Raila Odinga  na kiongozi wa walio  wengi bungeni  Aden Duale kwa kujadili  BBI  na Punguza  Mizigo mtawalia . Kupitia ujumbe huo Ruto amewakemea vikali  wanaojadili miswada wa Punguza Mizigo  na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka  wa 2022 .

Jopo la  Building Bridges Initiative  liliundwa baada ya mwafaka wa  ‘handshake’ kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila odinga .  Raila  mwezi uliopita alipuuza mswda wa punguza mizigo   na kuwaraia wakenya kungoja ripoti itakayotolewa na  jopo la BBI.  Wakati huo huo Duale wameunga mkono wazi  kurekebishwa kwa katiba ili kubadilisha mfumo wa  serikali .

Mbunge huyo wa Garissa mjini  amesema  ataunga mkono pendekezo la serikali yenye utawala wa bunge lenye maamlaka  il kumaliza ghasia za kila mara wakati wa uchaguzi wa urais . ODM ilikosoa mswada wa Punguza Mizigo ikitilia shaka jinsi tume ya uchaguzi IEBC ilivyothibitisha uhalali wa sahihi  zilizokusanywa  hasa baada ya juhudi kama hizo chini ya mpango wa Okoa Kenya mwaka wa 2017 kufeli wakati muungano wa CORD uliposhindwa  kupata sahihi halali zilizohitajika .