Google yachapisha orodha ya watu maarufu waliotafutwa sana 2019

Screenshot_from_2019_12_10_12_33_31__1575970441_33704
Screenshot_from_2019_12_10_12_33_31__1575970441_33704
Aliyekuwa bosi wa kampuni ya Safaricom Bob Collymore na mwanariadha Eliud Kipchoge wamekamata nafasi za kwanza katika orodha ya watu maarufu waliotafutwa kwa sana katika mitandao ya kijamii mwaka huu.

Bob Collymore alikuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom na aliaga dunia baada ya kupambana na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu.

Bob alijiunga na kampuni ya Safaricom Novemba 2010, na kuichukua nafasi yake Michael Joseph.

Bob na Eliud Kipchoge wana umaarufu mkubwa na pia mchango mkubwa katika jamii.

Kipchoge alitwaa ushindi mkubwa Viena, Austria kwa kuweka rekodi ya kimataifa kwa kukimbia kwa saa 2:01:39.

Aidha, Chuo Kikuu Cha Laikipia kilimtuza digrii ya maswala ya Sayansi wiki iliyopita.

“Leo nimepokea digrii yangu ya maswala ya Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Laikipia. Nashukuru familia ya vyuo vikuu kwa tuzo hii muhimu.” alisema Kipchoge.

Chuo hiki kilimtuza baada ya kuona juhudi wake na mchango mkubwa katika maswala ya spoti na michezo.

“Seneti hasa inamtambua kwa ufanisi wake wa hivi majuzi wa kuwa binadamu wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili,” Chuo Kikuu cha Laikipia kilichapisha.