Gor mahia kukabiliana na Green Eagles kwenye Robo fainali

Gor.Mahia
Gor.Mahia

Mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya Gor mahia watashuka dimbani hio kesho kuchuana na Green Eagles ya Zambia kuwania tiketi ya kucheza nusu fainali za Kagame cup kule nchini Rwanda. Mechi hio itaandaliwa ugani Umuganda Rubavu.

Gor ilifuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi D huku Green Eagles ikifuzu baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi C.

K'ogalo ni mabingwa mara tatu wa taji hilo.Kwenye hatua ya makundi, Gor mahia ilishinda mechi zake zote dhidi ya Maniema (2-1), AS Ports(2-0) pamoja na KMKM (1-0).

Mabingwa hawa mara kumi na saba wa ligi kuu nchini Kenya wanatumia mashindano hayo kujiandaa kwa mechi za CAF champions league pamoja na msimu ujao wa ligi kuu nchini Kenya.

Bingwa mtetezi wa taji hilo Azam atahitajika kupitia mtihani mgumu kwani atakabana koo na bingwa wa DR Congo, TP Mazembe kwenye robo fainali ya pili Ugani Stade de Kigali.

Mazembe walimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi A huku bingwa mara mbili mfululizo Azam akimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi B nyuma ya KCCA.

Mabingwa wa Rwanda Rayon Sport watachuana na na KCCA kwenye robo fainali ya tatu. Rayon sports ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi A nyuma ya Tp Mazembe. APR ya rwanda pia itachuana na Maniema ya CONGO

Mshindi wa taji hilo atapokea kitita cha US$30,000 huku nambari mbili akipokea US$20,000. Mshindi wa tatu atapokea kitita cha US$10,000.