Gor Semelang'o kutumikia kifungo cha siku 30 gerezani

Gor
Gor
Mfanyibiashara na aliyekuwa msimamizi wa hazina ya fedha za vijana Gor Semelang'o, atahudumia kifungo cha siku 30 gerezani kwa kukosa kulipa deni la mkopo ya shilingi milioni 3.6.

Semelang'o alitiwa mbaroni Jumanne alasiri na kupelekwa katika mahakama ya milimani Jumatano.

Mahakama ilimpata na hatia ya kushindwa kulipa deni hilo la mkopo na akahukumiwa kifungo cha mwezi moja gerezani.

Inaidaiwa kwamba alikopa fedha hizo kutoka kwa Lumumba Mumma & Kaluma Advocates. Nao walitaka korti iwasaidie kumshurutisha mfanyabiashara huyo kurejesha fedha hizo baada ya juhudi zao kuambulia patupu.

Semelang'o hakupewa nafasi ya dhamana hivyo basi hana budi kutumikia kifungo hicho.

Gor yupo katika Rumande ya Maeneo ya Viwandani.

Gor Semelang'o alitimuliwa ofisini kama msimamizi wa fedha za vijana na rais Uhuru mnamo Februari 27, 2014.