Siku ya Alhamisi mashabiki wa Rayvanny walishtuka baada ya kuamka na kupata akaunti ya msanii huyo haina picha yoyote na kushindwa nini kilitendeka ama ni jambo lipi lilimfanya afute picha zake.
Alitoa picha zote ambazo alikuwa ameweka kwenye mtandao huo na kuwaacha wafuasi wake millioni 4.9 bila majibu kwa mswali yao.
Hakuna anayefahamu nini chaendelea kwani mashabiki wake bado wamo gizani.
Hata hivyo, uvumi umekuwa ukienea kuwa Rayvanny amefanya hayo ili kutilia maanani albamu ambayo anataka kutoa. Wengine wanasema msanii huyo anataka kufunga kurasa zake za awali na kuanza maisha mapya.
Hizi hapa hisia tofauti kutoka kwa wafuasi na mashabiki wake;
C atwambie tu kuna kangoma kanakam
Hajadelete feed….He just deactivated his account temporarily
Kiki..though ni team Harmonize huyo.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO