Gunia la mabao: Southampton wakalifishwa 0-9 na Leicester

leicester city
leicester city

Leicester City hapo jana wali sawazisha rekodi iliyodumu kwa miaka 24 ya ushindi mkuu kuwahi andikishwa ndani ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuwakalifisha Southampton kwa mabao 0-9 katika uga wa St Mary's.

Southampton walilazimika kucheza na watu 10 baada ya kiungo wa Uingereza, Ryan Bertrand kuoneshwa kadi nyekundi baada ya dakika 12 kwa kumchezea pasivyo mshambulizi wa Leicester Ayoze Perez.

Ushindi huo uliwawezesha vijana wa Brendan Rodgers kupanda hadi nafasi ya pili baada ya kuipuku Manchester City katika jedwali huku wakisalia nyuma ya viongozi Liverpool kwa alama tano pekee.

Matokeo hayo yanayofanana na ushindi wa Man United wa 9-0 dhidi ya Ipswich mwaka wa 1995, ulithibitishwa katika kipindi cha lala salama baada ya bao lake Jamie Vardy kupitia mkwaju wa penalty.

Vardy na Ayoze Perez walifunga mabao matatu kila mmoja.

Youri Tielemans pia alifunga bao lake la tatu la msimu huku James Maddison akiongeza bao kupitia mkwaju safi wa free-kick katika usiku ambao wachezaji na mashabiki wa Southampton, walishuhudia timu yao ikishuka hadi msingi wa ligi kuu.

Baada ya kichapo hicho, Southampton sasa watasafiri hadi nyumbani kwa Manchester City, siku ya Jumanne katika kipute cha kombe la Carabao kabla ya kurejea Etihad katika mechi ya ligi kuu, Jumamosi, 2 mwezi wa Novemba.

Leicester nao watasafiri hadi Burton katika mechi za kombe la EFL Jumanne kabla ya kuelekea Crystal Palace kwa mechi ya ligi, Jumapili tarehe 3, Novemba.