Gwiji wa soka nchini Joe Kadenge aaga dunia

Gwiji wa Harambee Stars Joe Kadenge ameaga dunia hii leo.

Kadenge alipumua kwa mara ya mwisho katika hospitali ya Meridian baada ya kupambana na ugonjwa wa kiharusi (stroke) stroke kwa mda mrefu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Abaluhya United ambaye alishinda ligi kuu mwaka wa 1996, amekuwa ndani na nje ya hospitali lakini aliaga dunia jumapili akipokea matibabu, kulingana na Familia yake.

Kadenge anatambulika kama mmoja wa wachezaji bora zaidi nchini na amefariki akiwa na miaka 84.

Kadenge alilazwa hospitalini Alhamisi ambapo alipelekwa na wanawe baada ya kupata shida ya kupumua akiwa nyumbani kwake siku ya Jumatano.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.