messi

Habanduki wala kwenda popote: Lionel Messsi kusalia Barcelona

Baba na wakala  Jorge wa mcheza soka gwiji Lionel Messi anaripotiwa kuthibitisha kuwa nyota huyo atasalia Barcelona hadi mwisho wa msimu wa 2020/21 Uropa.

Taarifa hizo zinawatia moyo mashabiki wa Barcelona baada ya kuwa na wasiwasi wakati Lionel Messi aliwajuza Catalans kwamba anataka kuondoka.

Messi ajinasua! Mchezaji Messi aihama Barcelona?

Lionel Messi alitoa uamuzi wake baada ya klabu yake kupigwa na Bayern Munich katika mechi ya Ligi ya Mabingwa magoli 8-2 na kuwatupa nje ya mashindano hayo.

messi-compressed

Ni ushindi ambao uliibua msukosuko kwenye klabu hicho huku wengi wakikejeli na kukosoa uongozi wa klabu cha barcelona.

Ronald Koeman aliteuliwa kuwa meneja wa barcelona baada ya aliyekuwa meneja Setien kufutwa na kutimuiwa na viongozi wa klabu cha Barcelona.

Hata hivyo, hatua hiyo ilishindwa kubatilisha uamuzi wa Lionel Messi ambaye alikuwa amehusishwa na kuhamia Manchester City.

Messi The great: Ashinda tuzo ya 7 ya golden Boot katika La Liga

Kulingana na ripoti ya Goal ikinukuu Mediaset, baba yake Lionel Messi, Jorge amethibitisha kuwa mkutano wake na viongozi wa Barcelona ulikkwenda sambamba.

lionel messi

Hatma ya Messi uwanjani Camp Nou umekuwa ukizua gumzo miongoni mwa wachanganuzi na mashabiki wa soka kote ulimwenguni tangu wiki jana.

 

Photo Credits: hisani

Read More:

Comments

comments