Habari Muhimu Toleo la saa Moja 14/10/2019

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
Mgane wa  marehemu gavana wa Bomet Joyce Laboso,  ameteuliwa kuwa  mwanachama wa kamati ya ushauri kuhusu mashirika ya serikali .katika  uteuzi uliotangazwa  na rais Uhuru kenyatta kupitia arifa maalum ya gazeti rasmi la serikali  Edwin Abonyo  atakuwa mwanachama wa kamati hiyo kwa miaka mitatu ijayo. Abonyo ni miongoni mwa watu saba walioteuliwa .kwingineko waziri wa leba Ukur Yattani amemteua mbunge wa zamani wa Othaya Mary Wambui kuwa mwenye kiti  maamlaka ya  kitaifa ya ajira  kwa kipindi cha miaka mitatu .

Wenye magari watapata afueni mwezi huu baada ya mafuta ya petroli na diesel kupungua kwa mujibu wa tathmini mpya iliyotangazwa na tume ya Petroli na kawi . lita moja ya  petrol hapa jijini itauzwa kwa shilingi 108 Nukta 05 kutoka shilingi  112 na senti 81 .lita moja ya disel itauzwa kwa shilingi 101 na senti 96 kutoka bei ya awali ya shilingi 103 nukta 03 . bei ya mafuta taa hata hivyo imepanda hadi shiingi 101 nukta 08 kutoka shilingi 100 na senti 64 .

Bunge la  Kaunti ya Busia ndilo la hivi punde kuukata mswada wa punguza mizigo uliopendekezwa na chama cha Thirdway Alliance .waakilishi wa kaunti wamesema wananchi hawakuhusishwa katika kutayarisha mswada huo na vile vile utarejesha nyuma hatua zilizoafikiwa kufanikisha ugatuzi .

Chuo kikuu cha Moi Kimewafurusha  viongozi watano wa wanafunzi  ambao wanadaiwa kupanga maandamano yaliokumbwa na ghasia wiki jana  na kusababisha chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana .  naibu chansella Isaac Kosgey  amethibitisha kwamba wanafunzi hawatakubaliwa kurejea shuleni humo .

Mahakama moja mjini Voi imempata na hatia mwanamume mwenye umri wa miaka 56  aliyembaka  bintiye mwenye umri wa miaka 17.Mwemba Gereza anadaiwa kutekeleza kitendo hicho Agosti 28 mwaka 2016 katika eneo la Buguta huko Voi.Hakimu mkaazi wa Voi Fredric Nyakundi amesema upande wa mashtaka ulidhibitisha kuwa mshukiwa alitekeleza kitendo hicho cha kinyama

Chama cha ODM kimetakiwa kuwahakikishia wakenya kwamba kitadumisha amani wakati wa uchaguzi mdogo wa kibra .mbunge wa  kiharu Ndindi Nyoro  amesema kisa kama  kilichotokea mwishoni mwa wiki ambapo msafara wa mgombeaji wa Jubilee Mcdonald mariga ulishambuliwa kwa mawe  sio jambo linalofaa kukubaliwa .

Serikali itazidisha mara dufu jitihada za kukabiliana na udanganyifu katika mitihani ya kitaifa mwaka huu .afisa mkuu mtendaji wa  baraza la kitaifa la mihani Mercy Karogo  amewashauri  maafisa wakuu wa elimu katika kaunti ndogo kuhakikisha kwamba  wanafuatilia kikamilifu   usimamizi   wa zoezi la mtihani katika maeneo yao .