WIZARA YA elimu imefutilia mbali leseni za kuhudumu za shule mbili hapa nairpobi kwa ajili ya hofu kuhusu usalama wa shule hizo . waziri wa elimu George Magoha ameagiza kufungwa kwa shule ya Precious talent mtaani dagoretti ambako wanafunzi wanane walifariki katika mkasa wa kuporomoka kwa jengo na Pama academy mtaani kangemi . wanafunzi zaidi ya 400 waliokuwa precious talent watahamishwa hadi katika shule za msingi za Ngong forest , jamhuri na Riruta statellite . Mmiliki wa shule ya precious talent Moses wainana amekamatwa na atafikishwa kortini kesho .
kwingineko
Taarifa kutoka wizara imesema shule hiyo imewasajili wanafunzi wengi kuliko idadi inayohitajika ,haina vyoo vya kutosha hatua inayohatarisha afya ya wanafunzi na imejenga majengo yasio salama kwa wanafunzi . maneja wa shule hiyo pia ametajwa kama asiyehitimu kuisimamia .
Mahakama moja hapa jijini imekataa ombi la mkurugenzi wa mashtaka ya umma kubadilisha masharti ya bondi ya mfanyibiashara Humphrey Kariuki ili aweze kuzipata paspoti zake . DPP alitaka kariuki arejeshewa dhamana ya shilingi milioni 11 aliolipa kama pesa taslimu na badala yake atoe bondi ya thamani ya juu lakini mahakama imesema kariuki atalipa bondi itakayohakikisha kwamba atarejea kortini kuhudhuria vikao vya kesi yake .
Maafisa wakuu wa usalama katika kaunti ya Kiambu wamehamishwa mara moja kufuatia ongezeko la visa vya uhalifu katika eneo hilo .waziri wa usalama wa ndani Fred matiangi amesema watakabiliana na magenge ya uhalifu katika kaunti hiyo bila huruma .
Mswada wa Punguza Mizigo umekataliwa na bunge la kaunti ya Kisii na kuwa kaunti ya tano kuukata mswada huo . waakilishi wadi waliutaja mswada huo kama wa kupoteza muda na unaohujumu jitihada za kuzidisha uakilishi . kaunti za kirinyaga ,homabay ,nyamira na muranga ndizo ziliukata mswada huo wa irdway Alliance ilhali Uasin Gishu ndio kaunti pekee iliyoupitisha .
Siku moja tu baada ya afisi ya fedha ya kaunti ya busia kuteketea kwa njia ya kutatanisha, maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC wamevamia afisi ya gavana na kuchukua stakabadhi kadhaa.Maafisa hao saba walioandamana na maafisa wa upelelezi kutoka kaunti ya busia wamepiga kambi katika afisi hizo na kuonekana wakipekua stakabadhi kabla ya kuondoka nazo
Mahakama imemzuia gavana wa uasin Gishu Jackson Mandagapo dhidi ya kuongeza kodi ya ardhi . kaunti hiyo imepewa siku 14 kusuluhisha utata kuhusu suala hilo .Mandago hata hivyo amekanusha madai kwamba kodi ilitaka kuongezwa
Sarah Warimu, mjane wa bwenyenye mdachi marehemu Tob Cohen amehoji wajibu wa mkuu wa DCI George Kinoti katika kesi nzima ya mauaji ya mumewe .kupitia waraka aliowasilisha leo kortini ,wairimu amezua mswali kuhusu wajibu wa kinoti kuhusiana na mali alioachiwa dadake Cohen Gabrielle Van Straten. Kulingana na wairimu ,jukumu la Kinoti ni kuchunguza kesi ya uhalifu na sio umiliki wa mali .
Mmoja kati ya wanawake kumi Mombasa anataka kutumia dawa za kupanga uzazi lakini wengi hawawezi kuzipata dawa hizo . mkurugenzi wa afya katika kaunti hiyo Shem Phata amesema ni asilimia 55 ya wanawake ndio hutumia njia au dawa za kupanga uzazi .
Gharama ya dawa nchini ipo juu sana na kuna haja ya kuthibiti bei ya dawa ili kuhakikisha kwamba gharama ya jumla ya huduma za afya inapungua . Dr Kamamia Murichu kutoka kwa muungano wa wasambazaji wa dawa amesema dawa za humu nchini huuzwa hadi asilimia 200 zaidi ya bei katika mataifa mengine .
Polisi wamenasa mikebe 68bya plastiki iliyokuwa na cocaine pamojana sachet kadhaa za bangi mtaani riruta . oparesheni hiyo pia ilipelekea kupatikana kwa biskuti zilizotegezwa kwa dawa hizo .washukiwa wawili wamekamatwa na watafikishwa kortini .
MJANE WA bilionea Marehemu Tob Cohen Sarah Wairimu atasalia rumande hadi jumanne wiki ijayo baada ya kukosa kujibu mashataka ya mauai dhidi yake kufuatia ripoti kwamba wakili wake Philip Murgor ni na wakili wa mashataka wa serikali . jaji stela Mutuku amesema sarah atajibu tu mashjtaka dhi yake wakati suala hilo litaposuluhishwa .
Polisi wamenasa dola bandia za kimarekani na vipande 147 vya dhahabu Feki katika eneo moja la burudani mtaani kilimani hapa jijini . mmiliki wa eneo hilo amekamatwa .
Rais Uhuru Kenyatta amewarai wanachama wa umoja wa mataifa kuipigia Kenya kura katika azma yake ya kutaka kuwa mwanachama asiye wa kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwenye uchaguzi ukaofanyoka juni mwaka ujao . rais amesema Kenya imedhihirisha mchango wake katika kuleta amani duniani na kukabiliana na changamoto nyingine za kiusalama .
Serikali imesema itakabiliana vikali na wahalifu ambao wanawahangaisha wakaazi wa kiambu .waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi amesema atatekeleza mabadiliko katika idara za usalama katika kaunti ya kiambu .
Kuna ongezeko la idadi ya vijana wanaotumia mihadarati na pombe huko eldoret .kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Abdirizack Jaldesa amesema wamezidisha msako wa kuwakamata wanaouza dawa za kulevya kuwatumia watoto wa kuranda randa mitaani .