Mabunge ya Kaunti za Kisumu na tana river yameukataa mswada wa punguza mizigo . huko kisumu waakilishi wa kaunti waliukataa mswada huo baada ya mjadala wa saa moja wakisema kwamba unatishia kuhujumu katiba mpya iliyopitishwa mwaka wa 2010.katika bunge la kaunti ya tana river ,waakilishi wa kaunti wamesema kupunguza uakilishi sio jambo litakalowasaidia wakaazi wa eneo hilo.
Sarah Wairimu mjane wa Tob Cohen amewasilisha kesi kortini akitaka mkurugenzi wa DCI na DPP kuchukuliwa hatua kwa kukaidi agizo la mahakama .wairimu kupitia wakili wake Philip Murgor amesema wawili hao wamekiuka agizo lililotolewa na jaji Jessie Lessit kuwazuia kuzungumza na wanahabari kuhusu kesi ya mauaji ya mumewe .
Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai ameagizwa kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya vitendo vinavyokiuka sheria na uhalifu katika idara ya uhamiaji . Hii ni baada ya ufichuzi uliotolewa katika runinga ya Citizen kuhusu njama ya maafisa wa polisi na wale kutoka idara hiyo kutumia vitisho vya kumfurusha nchini mfanyibiasha mmoja wa asili ya kiasia ili kuichukua mali yake . msemaji wa wizara ya usalama wa ndani Wangui Muchiri amesema Mutyambai anatakiwa kuwasilisha ripoti ya hali ya uchunguzi wake ndani ya kipindi cha siku 14 .
Mbunge wa Tiaty William Kamket amewashtumu polisi kwa kutochukua hatua za kumtafuta mwanafunzi wa chuo kikuu aliyetekwa nyara katika kituo cha kawi ya mvuke cha olkaria ambapo alikuwa akifanya masomo ya kujifunza kazi . Kamket amesema mwanafunzi huyo alitoweka jana usiku mjini Naivasha wakati alipokuwa akiburudika na wenzake na amemshtumu OCPD WA eneo hilo kwa kujikokota katika jitihada za kuwakamata washukiwa .
Upo katika hatari ya kuhusika katika ajali ya barabarani siku za ijumaa ,jumamosi na jumapili kuliko siku yoyote ya wiki .Takwimu za NTSA ZAONYESHA KWAMBA watu zaidi ya 400 waliaga dunia katika ajali zilizotokea katika siku hizo kati ya januri na oktoba . watu 500 waliaga dunia siku za jumapili ,480 siku ya jumamosi ilhali 406 waliaga dunia siku za ijumaa .
Shirika la feri limeikabidhi familia ya marehemu Mariam Kighenda shilingi laki mbili ili kuisaidia familia yake kwa matayarisho ya maazishi yake na bintiye Amanda Mutheu . mumewe Mariam , JoHN WAMBUA PIA amepokea hundi ya shilingi elfu 682,500 kutoka kwa kampuni ya bima kwa gari lao lilitumbukia baharini na familia yake
Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amewaomba waajiri kuwaruhusu wafanyikazi wao wanaoishi Kibra kushiriki uchaguzi wa Novemba tarehe saba .Mudavadi amesema wenyeji wana wajibu wa kumchagua kiongozi ataayekamilisha kazi nzuri iliyoanzishwa na marehemu Ken Okoth .
Mzozo kati ya serikali na madreva wa magari ya mizigo unaendelea licha ya serikali kusema kwamba iliondoa agizo lililohitaji mizgo yote kusafirishwa kwa reli ya SGR .mfanyibiashara salim karama amesema hakuna kampuni ya uchukuzi iliyorejelea oparesheni zake .
Watu 400 zaidi wamefariki katika ajali za barabarani mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana katika kipindi sawa na hiki .takwimu za NTSA zaonyesha kwamba watu 2700 waliaga dunia kutokana na ajali za barabarani kufikia mwisho wa siku jana ikilinganishwa na watu 2300 waliofariki mwaka uliopita
Uteuzi wa mbunge wa zamani wa Othaya Mary wambui kama mwenyekiti maamlaka ya ajira umezua lalama kali sana mtandaoni kutoka kwa wakenya na hasa katika ukumbi wa twitter .wengi wamehoji nia ya serikali kumpa wambui kazi hiyo kwani suala la ajira linazua hisia kutoka kwa vijana wengi nchini ambao wamezua shauku iwapo wambui ana uwezo wa kutoa na kutekeleza sera na mikakati bunifu ya kuwawezesha vijana kupata kazi .waziri wa leba Ukur Yattani alitangaza uteuzi wa wambui katika maamlaka hiyi kupitia arifa maalum ya gazeti rasmi la serikali hapo jana .
Mwanamikakati wa mawasiliano ya kidijitali Dennis Itumbi na shahidi Samuel gateri wameshtakiwa upya kuhusiana na barua feki iliyodai kuwepo njama ya kumwua naibu wa rais William Ruto . wawili hao wamefikishwa kortini leo baada ya upande wa mashtaka kuziunganisha kesi zao . wamekanusha mashtaka ya kuchapisha taarifa ya wongo kinyume cha sheria .
Mkurugenzi wa mashtaka ya umma amewasilisha kesi ya ukiukaji wa agizo la mahakama dhidi ya mjane wa TOB COHEN SARAH WAIRIMU NA wakili wake Philip Murgor . DPP anasema wawili hao wanafaa kuchukuliwa hatua kwa kuzungumzia mauaji ya COHEN wakati wa maazishi yake .
Afisi ya mratibu wa bajeti imekashifiwa leo na maseneta kuhusu kutolewa kwa pesa kwa njia isiofaa kwa ununuzi wa vifaa vya matibabu katika hospitali za umma . aliyejipata pabaya ni kaimu mratibu wa bajeti Stephen Masha .
Mafuriko na maporomoko ya ardhi yanatarajiwa kukumba maeneo ya pwani na kati kuanzia alhamisi wiki hii .hata hivyo nairobi itakuwa na vipindi vya jua na mawingu kuanzia kesjo huku manyunyu ya mvua yakitarajiwa katika baadhi ya maeneo .huyu hapa bernad chanzu kutoka idara ya utabiri wa hali ya anga .
Zaidi ya hekari 1800 za mashamba yaliokuwa yamenyakuliwa yamerejeshwa kwa serikali katika eneo la Delamere huko Naivasha . afisa mkuu wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi twalib Mbarak amesema hilo limeafikiwa baada ya makubaliano ya nje ya mahakama na waliokuwa wameyanyakua mashamba hayo .
Vifo vya abiria bado vipo juu katika barabara zetu .takwimu za NTSA Zinaonyesha kwamba watu 1,050 waliaga dunia kufikia mwezi huu ikilinganishwa na 900 waliofariki mwaka jana kipindi kama hicho.
Waandamanaji wanaopinga SGR huko Mombasa wametahadharishwa dhidi ya kuvuruga sherehe za mashujaa .kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amesema mkutano wowote unaopangwa kufanywa katika uwanja wa tononoka siku ya mashujaa hautakubaliwa .
Madreva wa magari ya kibinafsi bado ndio hatari katika baraara zetu .takwimu kutoka NTSA zinaonyesha kwamba magari ya kibinafsi yalisababisha vifo vya watu 722 kati ya januari na oktoba mwaka huu ikilinganishwa na watu 630 waliouawa na magari ya kibiashara . madreva wa matatu walisababisha vifo vya watu 415 ikilinganishwa na watu 433 mwaka jana .Emmanuel Nabiswa anaripoti .
Bunge la kaunti ya meru leo linajadili mswada wa punguza mizigo .mswada huo hadi kufikia sasa umekataliwa na kaunti 16 na ni uasin Gishu pekee ndio iliyoupitisha .
Rais wa zamani wa afrika kusini Jacob Zuma atakata rufaa katika kesi ya ufisadi dhidi yake baada ya mahakama wiki jana kutupilia mbali ombi lake kwamba kesi hiyo ifutiliwe mbali . Madai ya ufisadi dhidi ya Zuma ni ya miaka ya 90 wakati taifa hilo lilipotoa kandarasi ya ununuzi wa sulaha .Hilo linajiri baada ya marekani wiki jana kuiwekea vikwazo familia ya Gupta na mshirika wao mmoja kwa tuhuma za ufisadi nchini afrika kusini . Familia ya Gupta ilikuwa na uhusiano wa karibu na Zuma na utawala wake.