COTU yataka wanachama wake kuongezwa mishahara

Picha: kahawatungu.com

Muungano wa vyama vya wafanyikazi COTU umewataka wanachama wa  vyama vyake tanzu kuitisha nyongeza ya mishahara na marupurupu kutoka kwa waajiri, ili kuwawezesha kumudu hali ngumu ya uchumi.

Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema malipo ya sasa hayawezi kustahimili ongezeko la bei za bidhaa na gharama za huduma kama vile usafiri na kodi za nyumba.