PATANISHO: Nalaumu Bangi Kwa Kunikosanisha Na Mke Wangu

steve
steve
Wanaume kwa wake, wengi hulimbikizia lawama chochote kilichokaribu nao ili kujikwamua kutoka kwa hukumu yoyote ile, iwe ni kazini au pia kwenye ndoa.

Mojawapo ya mengi yanayolengwa nyakati nyingi ni dawa ya kulevya aina ya bangi ambayo imekuwa chanzo cha madhara mengi katika jamii. Basi tukio hili lilitokea hapo jana katika kitengo cha Patanisho wakti bwana Collins alipolaumu bangi kwa kumkosanisha kati yake na mkewe.

Bwana Collins mwenye umri wa miaka 25, aliomba apatanishwe na mkewe Lydiah 23, baada ya wapendwa hao wawili kukosana mwaka uliopita, kisa na maana Collins alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe kila alipovuta bangi.

"Nilikuwa natumia bangi, katika harakati ya kuivuta jioni na marafiki, kufika kwa nyumba yangu ile bangi ilikuwa inanionesha sitaki kuona mwanamke yeyote karibu nami, hadi nikimuona mke wangu namtafutia makosa ili nimpige na hapo ndipo mke wangu hutoweka kwa masaa matatu. Bangi ikishuka kiasi nashtuka baada ya kugundia nilichokifanya na hapo ndipo namtafuta na baada ya tukio kadhaa mke wangu akadai amechoshwa na tabia zangu akidai napenda raha. Kurudi nyumbani baada ya siku kadhaa nikapata mke ameenda na akabeba vitu kadhaa na kumtafuta akawa mkali zaidi. Tumeishi kwa miaka miwili na aliingia kwa ndoa na mtoto mmoja."

Alisema bwana Collins huku akifichua amevuta bangi kwa miaka kumi kwani alianza tabia ile akiwa shuleni huku akikiri kuwa amewacha bangi na sasa ana miezi mitatu tangia aitumie.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be