PATANISHO: Ugali ndio ulitutenganisha na mume wangu

ugali (3)
ugali (3)
Lydia aliomba apatanishwe na mumewe akidai "Nimekosa tu kidogo ya nyumba, nakuanga na kibanda na siku moja nilikuwa nimewasha jiko kwa nyumba na nikawekelea maji.

Maji ilipochemka akaniita na kwa kuwa nilikuwa namalizia kazi fulani nikamweleza amwage unga mle ndani nitakuja kusonga ugali na hapo akakasirika na ile sima hakula.

Isitoshe, kesho yake akaamka na kukunja nguo zake na kwenda zake huku akiniwachia watoto wetu watatu." Alieleza Lydia ambaye wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na mitano.

Wawili hao walitengana mwezi wa tisa mwaka uliopita na Lydia anadai kuwa kila tunapozungumza hatuelewani kwani hunieleza nitafute bwana mwingine.

Josphat naye alikata simu baada ya kuzungumza nasi kwa mda mchache.

Alipokubali kuzungumza nasi alidai kuwa alikerwa na tabia ya mke wake kumpa majukumu za kupika chakula kwa nyumba. "Yeye nilimuachia duka lakini akiona kama ameshindwa na watoto aniletee nitashughulikia." Aliongeza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be