Dunia Ina Mambo! "Nilitoka Kwa Ndoa Baada Ya Baba Mkwe Ku Pupu Kwa Nyumba Yetu"

anita.raey
anita.raey
Je mke au bibi yako ashawahi fika mahali na kuamua kukunyamazia?

Na kama hilo lishawahi tendeka ni kosa lipi ulikuwa umefanya? - Hayo ndio yaliyokuwa maswali kutoka kwa Annita Raey katika kipindi cha Sema na Raey.

Mwanamke mmoja aliwashangaza wengi alipofichua kuwa baba mkwe ndiye aliyesababisha utengano wa mda kati yake na mumewe baada ya ku pupu au ukipenda kujisaidia ndani ya nyumba yao.

"Mimi nilinyamaza hadi nikatoka nilinyamaza kwa sababu father in law alienda aka pupu kwa nyumba yangu. Father in law alienda kwa nyumba yangu yenye tumejenga na kijana wake na ku pupu ndani. Alisimulia.

Sikuelewa mbona alifanya vile kwa sababu mimi na mwanawe tulikuwa kwa ndoa ya miaka kumi na minne. Kwa kimila yetu ile ni kama uchawi na bwanangu kwanza alidhani nilikuwa namsingizia lakini yote yalikuja yakabainika." Alieleza mwanadada yule huku akimuacha Annita Raey na wasikilizaji wote vinywa wazi.

Pamela kutoka maeneo ya Dagoretti pia alichangia mada ile huku yeye akidai chanzo cha kumnyamazia mumewe kilikuwa swala la mpango wa kando.

"Nakuambia mimi siwezi nyamaza kwa nyumba kwani nishawahi toka kwangu kwa ajili ya mpango kando. Siku moja niliguza simu ya mume na nikapata mwanamke ambaye alikuwa anamuuliza kama amefika nyumbani, kumuuliza akadai hamjui.

Sasa nikaondoka na kwenda nyumbani na huko nikampigia yule mwanamke na akakubali kunihadithia mambo yao yote na isitoshe siku moja akimtumia yule mwanamke ujumbe ule ujumbe ukaja kwa simu yangu na hapo akawacha zile tabia baada ya kumkemea. Aliongeza Pamela.

&feature=youtu.be