Msanii Ali Kiba afichua jinsi alivyokutana na mkewe nchini Kenya (AUDIO)

Ali Kiba ambaye yuko nchini kwa mikutano ya kuhakikisha kuwa uzinduzi wa kinywaji chake ' nchini Kenya utakuwa timamu, aliweza kuketi chini na mtangazaji Massawe Japanni siku ya Jumatatu.

Mwimbaji huyo ambaye alitamba baada ya kuzindua wimbo wake 'Cinderella' takriban miaka kumi iliyopita, alizungumzia maswala mengi katika mahojiano yake lakini kilichofurahisha wengi ni pindi alipofichua jinsi alivyo patana na mkewe Amina.

Ali Kiba alifunga pingu za maisha na mpenziwe wa siku nyingi, Amina Khalef Aprili mwaka huu katika sherehe ya kukata na shoka, katika uga wa Diamond Jubilee, Mombasa. Sherehe hiyo ili walete watu mashuhuri akiwemo gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Lakini wawili hao walipatana wapi?

"Ushawahi skia msemo unaosema mapenzi ni majani huota kokote hata juu ya nyumba aisee. Mkee wangu nilikutana naye hapa Kenya mjini Nairobi. Alikuwa anasomea USIU na nikabahatika kuwa naye tukafahamiana tukawa marafiki kwa mda mrefu.

I believe alikuwa shabiki wangu na alikuwa anapenda mziki wangu kwa mda mrefu. " Alieleza Ali Kiba.

Alipoulizwa iwapo mkewe anahofia kuwa jinsi alivyopatana na star huyo ndivyo huenda akapatana na mwanadada mwingi humo nje, alisema;

"Ki ufupi anaelewa jinsi maisha yangu yalivyo na ananijua vilivyo ananiheshimu na ananipenda nami nampenda sana.

Hiyo haina shida kwani anaelewa mume wake ni mtu wa aina gani, ni msanii na nashukuru kuwa anajiheshimu ndio maana mpaka sasa hivi hukuskia chochote kimetokea iwapo ni mda mfupi." Alisema.

Miezi saba baada ya wawili hao kuoana, wapendwa hao wawili tayari wanatarajia mtoto wao wa kwanza ambaye atakuwa mtoto wa nne wa msanii ambaye ana watatu na wanawake watatu tofauti.

"Katika dini yetu we believe kwamba ni faida kubwa ya ndoa wakati tumemaliza kufunga ndoa tukikaa kidogo tupate baraka. Mungu akipenda atajifungua mwakani lakini bado hatujui kama ni wa kike.

Wakati mwingine hufika na huwezi ishi na mtu bila makubaliano so ni ivo tu. Naishi na mtoto mmoja ambaye nilimchukua akiwa na miezi sita. Mwingine ambaye ni first born anaishi UK mwenye umri wa miaka tisa na wa mwisho ana miaka mitano."

Yafuatayo ni baadhi ya maswali mengine ambayo aliweza kujibu.

Je wataka kuingia kwenye siasa nchini Kenya?

Kiba: Hapana sina nia ya kuingia kwenye siasa, hizo ni fununu tu.

Changamoto gani kubwa umepitia?:

Kiba: Challenges ziko nyingi lakini siku yangu ya harusi kuna vitu vilitokea kama kuna watu nilitarajia watakuja lakini baada ya harusi nilipata lawama nyingi sana, 'kwa nini hukunialika na kadhalika'. Halafu maybe on social media kuna vitu ambavyo wengi hunizungumzia.

Pata mahojiano yote kati ya Ali Kiba na Massawe Japanni katika kanda ifuatayo.