PATANISHO: Gidi ambia huyo mwanaume tupatane 2021 simtaki sahii

Bwana Joseph ambaye alikosana na mkewe na mama wa watoto wao, bi Janet, mwaka jana msimu wa Krisimasi, alituma ujumbe akiomba apatanishwe kabla mwaka uishe.

Bwana Jose ana umri wa miaka 32 huku miaka akiwa na miaka 28. Wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa miaka minne.

"Sasa niliondoka nyumbani kwenda town msimu wa Krisimasi kutafuta nguo na nikapatana na mwanadada fulani, jirani fulani akaniona na akatoka mbio na kueleza bibi kuwa amezubaa na amenyang'anywa bibi.

Bahati mbaya bibi akaja na nilipomuona nikahepa hadi nyumbani. Mke wangu akaleta hasira nyingi na tukakosana sana. Sahii nimeteseka kwa maneno ya kuosha vyombo, kufua na maneno mengine ni ngumu." Alijitetea Jose.

Wawili hao wamejaliwa na watoto wawili ambao sahii wako na mama yao.

"Wewe si unajua ulichonifanyia? Mimi nilikuwa nakupenda sana lakini sasa wewe mwenyewe hapana." Bi Janet alisema akidai kuwa alimpata mumewe akiwa na mwanadada mwingine.

Mimi nakwambia unipatie miaka mitatu ili nitulie kwani roho yangu bado ina hasira. Naomba anipe miaka mitatu lakini asije akaoa mke mwingine, aningoje." Aliongeza Janet.

Pata uhondo kamili.

&t=3s