PATANISHO: Bwanangu alikatwa kichwa na mpango wa kando na bado akamrudia

Bwana Charles, aliyewachwa na mkewe takriban miaka miwili iliyopita kwa kuwa na uhusiano wa kando na mke wa mwenyewe, alituma ujumbe akiomba apatanishwe.

Isitoshe, alifichua kuwa alikuwa kwa uhusiano na mwanamke mwingine kwa mda wa miaka mitano bila mkewe kufahamu, na cha kushangaza ni kuwa wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Soma usimulizi wake.

Bwana Gidi, ilikuwa wakati mmoja nikawa na mpango wangu wa kando takriban miaka mitano ivi na tulikuwa pamoja kwa miaka miwili kabla mke wangu kujua. Na alipojua, mimi na yule mpango wa kando tulikuwa tushafanikiwa na mtoto.

Mke wangu alipojua alikasirika lakini nikamuongelesha na akatulia kidogo nami nikaenda kazi nje. Nikiwa kule aliposikia bado naendelea na huyu mpango wa kando, akafunganya virago na kwenda kwao nyumbani. Sasa imetimia miaka miwili tangia aondoke na hajawahi rudi.

Charles alidai kuwa mkewe Salome, ambaye pamoja wamejaliwa watoto wanne wamekuwa wakizungumza lakini hataki kumrudia licha yake kushughulikia watoto wake.

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka tisa.

Hakuna kitu naweza kukusamehea, hakuna kurudi! Sirudi na sirudi. Bi Salome alisema pindi tu aliposkia sauti ya aliyekuwa mumewe.

"Alinitesa sana alinitesa hadi nikifikiria bado nina hasira, alinitesa sana hadi nina ma alama za kunipiga. Nimevumilia sana kwanzia 2013 mpaka wa leo, nilikuwa hata karibu kujiua na watoto lakini nikasema wacha tu nitoke huko kuliko kujiua." Alieleza Salome akidai kuwa Charles alikuwa hadi na tabia ya kumpiga mamake mzazi.

Pata uhondo kamili.