Waakilishi wa wadi ya Nairobi wamwambia Waititu mjini si kaunti ya Kiambu

1882330(2)
1882330(2)
Wawakilishi wa kaunti ya Nairobi jana walimkosoa gavana wa Kiambu Fredinand Waititu kwa kuwauliza wakikuyu ku mteuwa mmoja wa wao kama gavana wa kaunti ya Nairobi mwaka wa 2022.

Waithaka Antony Kiragu pamoja na wenzake walisema Nairobi ni kaunti ya ustaarabu. Waititu aliyasema maneno hayo mwishoni mwa wiki.

Waakilishi hao wakiongea na maripota katika chumba cha city hall, walimuhukumu gavana huyo wakusema kuwa matatu za watu 14 hazijakaribishwa na zipigwe marufuku mara moja.

Serikali imepiga marufuku leseni mpya za matatu 14 katika mji wa Nairobi. Waititu alisema marufuku hayo yanapaswa kusimamishwa kwa miaka zingine 10.

Sheria kuzuia matatu za watu 14 (14 seater) kutoka mji ilipitishwa  mwaka wa 2016 wakati gavana Waititu alikuwa mbunge wa Embakasi.

"Swala hili halina chochote cha kufanya na mji,"Kiragu alisema.

Marufuku hayo yangefanya kazi mwezi wa Desemba mwaka wa 2016 lakini Rais Uhuru Kenyatta akisimamisha kwa miaka miwili.

Kiragu alisema Waititu amekuwa kikwazo katika jitihada kwa ajili ya utaratibu na mfumo wa usafiri. Marufuku hayo yamefanyika ili kuongeza na kuimarisha usalama.

"Tunafahamu vyema Watitu juu ya machafuko na wazimu lakini hatutakabali hili katika mji," Kiragu aliongeza.

Mwaka uliopita Waititu alimuuliza gavana wa Nairobi Mike Sonko awache ubomoaji wa manyumba zilizokuwa kuwa karibu na mito, lakini asongeshe njia za mito.

Sonko alimwambia na kumuuliza awache kuingililia mambo ya kaunti ya Nairobi. Wawakilishi hao walimwambia Waititu azingatie kaunti ya Kiambu.

Kaunti ya Nairobi si ugani wa kiambu," mwakilishi wa Roysambu Peter Warute alisema.