Bosi wa benki ya DTB akanusha madai ya kuhusika na shambulio la DusitD2

soppic
soppic
Meneja wa benki ya DTB, ambaye ni mshukiwa mkuu wa kuwawezeshesha maigaidi kwa kuwapa fedha ili kukamilisha  shambulio lao la DusitD2 kaunti ya Nairobi, amekanusha madai kuwa hakuhusika katika kuwapa fedha magaidi hao wala kuwezwsha.

Meneja huo alitaka kuachiliwa katika mikononi mwa polisi. Ilhali ilisemekana akuwe katika mikononi mwa polisi kwa siku 30 zaidi.

Meneja huyo wa benki hiyo Sophia Njoki Mbogo alisema kuwa hakuna watuhumiwa wa ugaidi ambao wako na akaunti na benki hiyo.

Sophia aliongezea na kusema kuwa hajawahi kabiliana na magaidi hao kikazi ama kwa hali ingine yeyote.

" Mimi sina hatia yeyote katika uchunguzi huu wa jinai,na sina uhusiano wowote na washukiwa hawa watano wa shambulizi hilo,na mimi na heshimu sheria na sina rekodi yeyote na polisi." alisema Sophia.

Mama wa watoto wawili jumatano aliletwa mbele ya hakimu mwandamizi mkuu Martha Mutuku pamoja na Hassan Abdi, Ismael Sadiq Abitham, Ali Khamisi Ali, na Abdinoor Maalima Osmail.

Polisi walimtuhumu kama bosi wa tawi kwa kuruhusu kiasi kikubwa kutolewa bila swali lolote.

Kuhusu utaoji wa kiasi kikubwa cha pesa, Sophia aliambia mahakama kuwa benki hiyo inatumika kama wakala wa mtoa huduma za mawasiliano na kukubaliwa utoaji wa pesa kama ilivyo agizwa na kampini.

Bwana Abitham inaaminika kuwa aliwasiliana na mhusika mkuu wa shambulizi hili Ali Gichunge, ambaye aliweza kufariki kufatia makabiliano yao na polisi na mkewe ambaye bado hajulikani alipo.

Osmail ambaye alipokea laki 100,000 kupitia mtandao wa Mpesa, pia yuko mikononi mwa polisi huku mahakama ikisema kuwa pesa hizo zilikuwa zimetoka kwa waliohusika katika shambulizi hili.

Hassan, mwanabiashara katika maeneo ya Eastleigh, inaaminika kuwa aliwasiliana na gaidi aliyehusika katika shambulizi la Garissa bwana Faisal Mohammed Digale na gaidi Ali Gichunge, aliyehusika katika shambulizi la DusitD2.

Washukiwa kumi na 16 sasa wako mikononi mwa polisi kuhusiana na shambulizi ambalo lilisababisha vifo vya watu 21.

Pia Nur ameshtakiwa kwa kupokea shillingi millioni 9 kisha akazitoa kupitia Mpesa nchini Somalia.