Ilikuaje: Guardian Angel aeleza jinsi alivyoteseka baada ya kukataliwa na babake

Mwanamziki Guardian Angel almaarufu Audiphaxad Peter amelelewa na mama peke yake kwa maana aliweza kukataliwa na baba yake akiwa bado hajazaliwa.

Ni mkristo ambaye amepitia mengi kisha kuja kuwa mwanamziki maarufu wa nyimbi za injili.

Guardian amekuwa akiimba kwa miaka nane mwaka wa 2017 ndivyo alivyojulikana mzuri na mashabiki wake.

"Ilifika kiwango mpaka nikasikia kuacha kuimba nyimbo za injili kwa maana nilikuwa naona nyimbo hizo zingine ziko na mashabiki wengi kuliko za injili hasahasa zangu.

"Nilikuwa nimepanga niimbe wimbo wangu wa mwisho kisha niwache lakini na mshukuru mungu hakuniacha," Alisimulia Angel.

Walipokuja Nairobi na mamake kazi iliisha na kuanza kuteseka tena ndipo alipo rudi mitaani tena hili kujikimu, alikaa mitaani kwa miaka miwili.

"Nilikuwa nishaa zoea maisha ya mitaani kwa hivyo nilitoka nyumbani nikaenda mitaani tena lakini mamangu hakujua ama nimerudi mitaani tena," Aliongea Guardian.

Mama yake aliweza kuongea na babake mzazi wa Angel akiwa na miaka kumi ilhali hakuwasaidia na chochote.

Baada ya miaka miwili rais Uhuru Kenyatta kuamuru vijana wote ambao wako mitaani washikwe na kupelekwa shuleni mwa mayatima.

"Baada ya rais kuamuru tupelekwe shuleni mimi nilienda baroni kwa miezi miwili kisha nikapelekwa 'Approved school' baada ya hapo tuliweza kuambiwa ambao wanajua kwao wapelekane ili kuona jamii zao," Alisema Angel.

Baada ya mwana mziki huyo kutoka shuleni, waliweza kuhama Kibera kisha wakaenda Mwiki na mamake ambapo maisha yalikuwa magumu zaidi.

"Niliokoka nikiwa jela na kutoka nikue mndogo mama yangu alikuwa mkristo, huwa naomba sana katika maisha yangu," Alizungumza Angel.

Angel ni mwanamziki ambaye hajaoa, aliweza kusema kuwa wana mziki wengi huwa wanaimba tu ili waweze kuonekana lakini si kusambaza injili ya yesu.

Baada ya kutoka 'approved school' Guardian alirudi nyumbani ili aweze kukamilisha masomo yake. Alipofika kidato cha tatu aliweza kutoa wimbo wake wa kwanza ambao unaitw 'Amaizing grace'.