PATANISHO: Nilifungwa jela na watoto baada ya mke wa tatu kuleta kisirani

patanisho.
patanisho.
Teresiah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Mbuvi.

"Hata sijui tunakoseana nini na mzee kwani 2017 Disemba alibeba vitu vyote na kuhepa kwa nyumba na kuniachia mtoto." Alieleza Teresiah.

Sasa alianza kurudi polepole na kusema anataka turudiane kama kitambo. Hata hivyo alitafuta mwanamke mwingine na kuanzisha maisha mapya na nilipomuuliza alisema kuwa atafanya anacho taka.

Juzi alibebana na mwanamke, bibi wa kwanza na kwenda nyumbani kwangu. Bibi kwa hasira akamuuliza mimi ni nani na hapo akamwagia mwanamke wa tatu chai." Alieleza akisema kuwa mke wa kwanza anamtambua kama mke wa pili ila hajui mke wa tatu.

Hapo Teresiah aliwekewa lawama na watoto wake na walifungwa jela kwa wiki kadhaa.

Wawili hao wamejaliwa watoto watatu kwa ndoa ya miaka kumi.

"Unajua shida yenye inafanya nisije wewe ulisema nikija huko utaniitia watu waniue, si wewe ulinipigia simu tarehe 25 ukinitishia. Nitatafuta siku nije tuzungumze sahii niko busy." Mzee Mbuvi alisema kabla ya kusitisha mawasiliano yao.

Unajua Gidi, nikienda huko nitampata mwanamke mnono kwani juzi nilimuacha na mkonde, sijui kama amerogwa au nini." Aliongeza Teresiah.

Alipojibu simu mara ya pili, Mbuvi alisema kuwa watoto wake aliosomesha sasa wamekuwa watundu na wanasema kuwa yeye sio baba yao. Isitoshe, wanawe sasa wamekuwa wezi na Teresiah alimuibia elfu arobaini na tano.

Pata uhondo kamili.