PATANISHO: Tulikosana na mke wangu kwa ajili ya mpango wa kando

Ian alituma ujumbe akiomba usaidizi ili apatanishwe na mkewe Bi Esther, ambaye walikosana miezi mitano iliyopita.

Kulingana na Ian walikosania maneno ya simu na tangia siku hiyo mkewe hajakuwa akijibu simu zake.

“Tukiwa kwa nyumba na mtu anipigie simu yeye alikuwa analeta shida. Nilikuwa nyumbani Bungoma nikifanya kazi ya bodaboda na kuna msichana tuliyepatana huko na tukawa na urafiki na akawa mpango wangu wa kando.

Sasa nilipopata kazi Nairobi alijua nilikuwa na mpango wa kando na licha yangu kuwachana naye, bado mke wangu alikuwa ananishuku”

Wawili hao ambao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano, wamejaliwa watoto wawili na walienda na mama yao.

Alipopigiwa simu bi Esther alidhibitisha kuwa wawili hao walikosania maneno ya simu lakini shida kuu ilitokea baada ya huyo mwanamke kuwatesa watoto wake.

"Hayo yote yalinifanya niamue kutoka kwake na kwenda nyumbani. Isitoshe ni mwanamke mkuu ki umri kumshinda na ana watoto karibu saba.

Nilienda kwa bwanake na akasema kuwa waliwachana baada ya yule mwanamke kuwaacha watoto wake." Alieleza Esther.

Naye Ian alijitetea akisema, "Hata sikuwa najua hayo, ningalijua ana watoto saba singekuwa nayeye, hii mafuta ilikuja wanajipaka wanakaa nyororo sasa huwezi jua."