Sababu za kutomueka baba wa mtoto wangu kwenye mitandao - Awinja

Muigizaji Jacky Vike anayefahamika kwa sana kama Awinja, alisema kuwa kutoweka kinachoendelea katika familia ama kukosa kuweka kuhusu familia yake kwenye mitandao kumemsaidia sana.
"Huwezi kuwa na furaha maishani, wakati waishi maisha ya uongo ili kuwapendeza watu kwenye motandao ya kijamii." Alisema Awinja.

Awinja ni muigiza wa televisheni katika kipindi kimoja ambacho kinafahamika na kujilikana kwa sana wananchi 'Papa shirandula' anaigiza kama mfanyakazi ambaye ana kelele nyingi.

Alisema kuwa huwa anataka kuwa mkweli na kuwa yeye inapokuja katika upande wa mitandao ya kijamii.

Aliongeza na kusema kuwa wanarika wengi, wanapotoshwa na vitu ambavyo watu mashuhuri huwa wanaweka katika mitandao ya kijamii.

"Ambacho huwa mnaona katika mitandao ya kijamii kunihusu kwa hakika si mimi, mimi ni mtu tofauti wakati siyuko katika mitandao ya kijamii,

"Ni jambo ambalo tumewachagulia watu waweze kuona." Aliongea Awinja.

Hata hivyo Awinja huwa anajaribu juu na china kuwa kama yeye katika mitandao ya kijamii, huwa haweki jambo lolote ambalo ako katika maisha ya juu, ambapo watu wanadhani hawezi ongeleshwa.

Alijifungua mwaka wa 2017, mtoto wake wa kwanza na akusema  kuwa kumembadilisha sana kuwa mzazi kwa sababu sasa anajua dhamana ya kuwa mzazi.

"Unapata kuwa na uzoefu na pia kupata upendo wa kweli, kuwa mama ni jambo nzuri sana siwezi kufikiria kuishi bila mtoto wangu,

" Mvulana wangu atakuwa na miaka miwili mwezi wa juni mwaka huu." Awinja alizungumza.

Licha ya kuwa na kazi nyingi Awinja hajakuwa naugumu wowote wa kulea mtoto wake, kwa sababu kazi yake rahisi na pia mama yake huwa anamsaidia kumlea mtoto wake.

"Unasoma ukiendelea, mama yangu huwa ananifunza na kuninyesha njia ya kufanya jambi." Alisema.

Machache yanajulikana kuhusu baba wa mtoto wake, na kusema kuwa huwa wanasaidiana kumlea mtoto wake.

"Ukweli kuwa huwa simueki baba wa mtoto wangu katika mitandao, haimaanishi kuwa hatuko pamoja, tunamlea mtoto wetu pamoja

"Ni kwa sababu huwa nachagua chochote ambacho nahitaji watu kujua kuhusu maisha yangu katika mitandao." Alisimulia Awinja.