PATANISHO: Mume wangu hunidunga visu tukipigana

Monicah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe baba Jeff, ambaye walikosana mwezi mmoja uliopita na wawili hao hawazungumzi, isitoshe mumewe alimwambia kuwa atamuua.

Tulikosana mwezi uliopita tarehe 21 na nimekuwa nikimshuku ana mpango wa kando na isitoshe amekuwa wa kunidunga na visu kila mara tunapigana.

Every Thursday huenda kazini na harudi kwa nyumba, kumpigia simu nikaskia echo na nikamuuliza kama yuko kazini kwani sikuskia mlio wa magari.

Sasa akanikelelesha akiniambia namchunga na akaniambia tupatane kwa nyumba eti nitamtambua. Kufika akanipiga na mshipi huku akisema kuwa nafaa kuhama na watoto. Alisimulia akisema kuwa anashuku hana mpango wa kando wala alioa bibi mwingine.

Monicah na mumewe wamekuwa kwa ndoa ya miaka na saba na wamejaliwa watoto wawili huku mmoja akiwa kidato cha tatu na mwngine akiwa darasa la sita.

Mwanadada alisema kuwa amejaribu kumuongelesha na ameshindwa isitoshe hamna yeyote anayeskiza na amejaribu kila juhudi na ameshindwa.

Juhudi zetu za kumtafuta bwana Ken hazikufua dafu.

&feature=youtu.be