PATANISHO: Sina wanawake wengine hao ni ma customers!

Diana alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Nicholas.

Ni mambo tu ya nyumba shida kidogo kidogo kutoelewana akija kwa nyumba tunagombana na ananiambia nitoke niende.

Sasa nikaona haya maneno ya kuambiwa uondoke kisha unafanyiwa maneno sitaki na nikaamua niondoke. Nili time siku moja ameenda job na nikafunganya virago na kuondoka wiki mbili zilizopita.

Siku moja alinipigia simu kuuliza niliko na nikamwambia yeye ndiye alinifukuza na kuwa hafai kuuliza niliko." Alisema Diana.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minane na hawajaliwa watoto. Diana anasema kuwa wakati bwanake alikuwa anataka mtoto yeye hakuwa tayari na sasa anavyotaka watoto mumewe hakuwa anataka.

Isitoshe wawili hao wana watoto kupitia ndoa tofauti lakini wanawashughulikia pamoja.

Bwana Nicholas alipopigiwa simu alisema;

Makosa ni yako kulingana na venye unaniongelesha, huwezi amini maneno ya simu bila evidence unaniwekelea vitu sijafanya na ndio maana nimekasirika.

Mimi nimetulia tu halafu nikifikiria nitakuambia.

Hata hivyo bwana Nicholas alikiri kuwa hana mipango ya kando kwani wanawake anaozungumza nao ni wateja wake.