Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

massawe Japanni likizo
massawe Japanni likizo

Wengi wa wasikilizaji wanajiuliza maswali mengi alikokwenda mtangazaji maarufu Massawe Japanni.

Mtangazaji huyu hajasikika kutoka juzi katika shoo yake. Mkali huyu huwa anayepeperusha kipindi kianchofahamika kama Bustani la Massawe kupitia masafa ya hewani ya redio Jambo.

Mashabiki wa kituo hiki cha utangazaji upendezwa zaidi na sauti yake inayotia fora zaidi. Idadi kubwa ya wasikilizaji wakiwa na maoni kuwa amepata kazi katika redio tofauti hapa nchini.

https://www.instagram.com/p/BwKuBjqBMef/

Mtangazaji huyu yupo katika likizo fupi na kwa ishara ya picha anazotupia katika mtandao wako rasmi na maridhawa wa Instagram zinaashiria yupo na familia nzima katika safari ya kula bata na kujisahaulisha uchovu wa kazini.

Kabla kupata kazi katika kituo cha redio Jambo alikuwa na shoo ya redio katika Milele FM. 

https://www.instagram.com/p/BwLkoapANnH/

Kipindi chake Massawe uhamasisha wana ndoa kuishi vizuri na kuwajibika kulea watoto. Huwapigia simu wanaume waliotelekeza watoto na familia zao na kulaani vitendo vya kuwapiga kuwadhulumu wamama katika ndoa.

Likizo yake inatazamiwa kuchukua muda wa siku 14 na arudi katika kituo cha utangazaji cha Redio Jambo kuzidi kuchapa kazi na kuwakonga nafsi wasikilizaji wake.

https://www.instagram.com/p/BwLq5TnA_Ui/