PATANISHO: Ukibadilika nitajua tu kwani CCTV Ni mob

Baba Mary belle aliomba apatanishwe na mkewe bi Mary belle, akidai walikosana tena na angepata apatanishwe.
Tulikosana mwezi ulioisha baada ya kwenda nyumbani na kumkosa. Nilipompigia simu aliniambia kuwa nafaa kufanya urafiki na pombe.

Sinywi pombe nyingi lakini si unajua mwanaume lazima apanguze vumbi akitoka kazini.

Sijamuoa ki rasmi kwani mimi ni generation ya microwave na ilikuwa tu ile ya come we stay.

Jamaa ana miaka 29 huku mkewe akiwa na miaka 23. Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitatu na tayari wana mtoto mmoja.

Anajua chenye alinifanyia na awachane tu na mimi, alisema mama Mary belle. 

Hata kama mungu aliamua tuwe pamoja hakuna mahali ali sign. Wewe ile time utawacha kuoa pombe na marafiki zako utanitafuta na ukibadilika nitajua kwani CCTV ni nyingi.

Alisema Serah akisisitiza kuwa mumewe akibadilika atarudi.

Mumewe aliongeza kuwa alianza kubugia pombe kutoka akiwa kidato cha pili na ameshindwa kuwacha kwani yeye hunywa akisombwa na mawazo.