Toboa siri: Bibi anadhani nilifariki ila nimekuwa kwa mpango wa kando

Toboa siri - mbusii
Toboa siri - mbusii
Kila siku ya wiki kuna kitengo cha 'Toboa siri' ambacho huletwa kwako na watangazaji hodari, Mbusii na Lion katika shoo kali ya Mbusii na Lion teketeke.

Katika kitengo hiki, waskizaji hupata fursa murwa ya kufungua roho na kusema kile ambacho wamekuwa wakibeba moyoni. Hii ni kuwasaidia kuomba msamaha na pia kuwasamehe waliowakosea.

Basi kuna jamaa ambaye alifichua kuwa familia yake inaamini kuwa alifariki na akazikwa, baada ya ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines.

Kulingana naye, mkewe alijua kuwa alisafiri hadi Ethiopia kikazi na alikuwa arudi tarehe kumi mwezi wa tatu, siku ambayo ndege hiyo ilianguka na kuua kila mmoja aliyekuwa ndani.

Cha kushangaza ni kuwa jamaa huyo baba wa watoto wawili, alimdanganya mkewe kuwa bado yuko Ethiopia ilhali alikuwa Nairobi kwa mpango wa kando.

Akiwa na mwanadada huyo, ndipo alipokea habari kuwa kumetokea ajali mbaya ya ndege, ndege ambayo mkewe alikuwa amengoja imrudishe mumewe nyumbani.

Hapo ilibidi familia yake ifanye shughuli za matanga na kuuzika mgomba wa ndizi kwani mwili wake haukupatikana. Hiyo ni kulingana na mila na desturi zao.

Sasa hajui la kufanya kwani ana huzuni na pia anataka kuirudia familia yake.

Soma usimulizi wake.

Nafanya kazi ya kuweka CCTV town na kuna hii tender ilitoka ya kwenda kazi Ethiopia.

Kazi ilipoisha siku yenye tulitoka Ethiopia nilimdanganya bibi yangu kazi haijaisha ila niko na mpango wa kando huku Nairobi.

Shida nilimwambia kuwa nitarudi tarehe kumi mwezi wa tatu na nikiwa kwa yule msichana tukaona ile ndege ilikuwa inatoka Ethiopia imeanguka na watu wote wamefariki. Hapo walijua kuwa nilikuwa kwa ile ndege na nilifariki.

Hapo walishiriki mambo ya matanga na wakaenda nyumbani na kuzika mgomba wa ndizi kama mwili haujapatikana.

Shida iko nataka kurudi nyumbani kwani baada ya kutoka kwa mpango wa kando nilikodisha nyumba na nikabadilisha nambari yangu. Mahali siko sina amani kwani mimi hutokwa na machozi nikikumbuka.