Hali ya umaskini yasababishia Ashley na Joyce kujitosa katika ukahaba

IMG_3699
IMG_3699
Katika kipindi cha Bustani La Massawe kitengo cha Ilikuaje, wageni katika studio walikuwa wawili Ashley na Joyce ambao wamekuwa katika uraibu wa ukahaba kwa muda mrefu. Wawili hawa wana sababu zao zilizowafanya wajitose katika kazi hii.

Soma mengine hapa:

Ashley, 22, baada ya kumpoteza mama akiwa kidato cha pili alipata pigo la kimaisha na kujipata katika tandabelua huku akilelewa na baba wa kambo.

Baba huyu ndiye alimuingiza katika ukahaba. Kazi hii alikuwa anaifanya ili kumsitiri kakake mdogo pamoja na mahitaji yake ya kila siku.

“Nilipoteza mama nikiwa kidato cha pili miaka minne iliypita. Hapo nikaanza kujipata katika matatizo kidogo. Babangu wa kambo alinipeleka katika danguro ili niingize pato la kila siku.”

Binti hawa wanasimulia jinsi wanavyojipata katika matatizo kazini yao huku wakitaja wanapolisi kama changamoto kubwa. Hali kadhalika wameweza kufunguka jinsi wapo katika mahusiano na wanapotumia ujanja kuwafanya wanaume wao wasijue kazi wanayoifanya.

Pata uhondo hapa:

Huwa wanapata kipigo kikali kutoka kwa wateja wao na wengine kukosa kuwalipa katika vyumba vya kukodi.

Joyce alianza ukahaba baada ya ufukara katika nyumba yao kukita mizizi.

Anasimulia kisa na ambapo alibakwa na marafiki wake wanne wakitoka shuleni na hapo akapata ujauzito.

“Nimelelewa na single mum na nyumbani tuko watoto watano. Mamangu anafanya kibarua na kuzungusha nguo. Ikafika kipindi tunatoka shuleni saa kumi na mbili mimi na marafiki zangu tukapatana na wanaume watano na wakatubaka na hapo nikapata mimba."

Hatimaye wawili hawa wamejutia kuwa maisha yao yalizama katika usiku wa giza totoro na kutoa nasaha kwa wanadada wasiufuate mtindo huu.

Soma hadithi nyingine hapa:

&t=602s