Ilikuaje: Nilimuua rafiki yangu nikiwa na miaka 15 - Stephen Kyenze

stephen chenza
stephen chenza
Jamaa kwa jina Stephen kyenze alisimulia jinsi alivyojipata amejitosa katika uhalifu akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu kupitia kushawishiwa na marafiki wabaya.

Akiwa mgeni wetu katika kitengo cha 'Ilikuaje' alieleza jinsi maisha yake yalivyobadilishwa na uraibu wake wa madawa za kulevya.

Fidel ni Mtu ambaye nimepitia mengi mambo ya madawa uwaji na nashukuru mungu wenzangu wameuliwa wako korokoroni nami niko huru na nina familia.

Nilianza 1993 nikiwa kijana mdogo kwani niliingizwa na marafiki kwa uhalifu kwani waliniambia niwabebee gunia za sukari ambazo walikuwa wameiba.

Alijipata amejitosa katika wizi wa mabavu ambao ulipelekea pia yeye kumuua rafikiye akiwa na umri mdogo. Kulingana na kyenze ambaye hakutaka kusimulia kile kisa kwa kuwa bado lile tukio bado humuuma.

Lakini cha muhimu ni kuwa yeye na familia ya rafikiye walisameheana kitambo na wao ni marafiki sasa hivi.

 Nimewahi kuua na niliua mtu mmoja kwani wakati huo nilikuwa nanywa mkorogo wa madawa za kulevya.

Sipendi kuzungumzia hilo jambo kwani wakati huo sikuwa naona likiwa jambo kuu lakini sahii nina regret. Nilishtakiwa lakini sikufungwa lakini singependa kuzungumzia jambo hilo.

Familia inajua nilichofanya na sasa sisi ni marafiki na huwa tunazungumza vyema kwani tulisameheana. 

Cha kushangaza ni kuwa kyenze na marafiki zake walikuwa wanashirikiana na afisa wa polisi ili kutekeleza uuzaji wa madawa na pia kuwaibia wananchi.

Katika uraibu wake wa wivi hapo ndipo alipatana na mke wake na wawili hao wakajaliwa watoto wawili katika ndoa iliyojawa na misukosuko.

Hata hivyo, wawili hao walikosana mwanao wa kitinda mimba akiwa na miezi mitatu lakini hadi wa leo hawajawahi patana na ila hajui aliko.

Baada ya miaka ya uhalifu, Ilifikia mahali na kyenze akaamua kubadilika na hapo akahudhuria ibada kanisani na akaombewa.

Sasa kyenze ambaye pia ni msanii wa uchoraji, ni mmoja wa wanao wasaidia vijana waliomo katika uhalifu kubadilika na kuanza kujitegemea.

Ilifika mahali nikaona venye marafiki zangu wanauliwa na raia na polisi, mara nimelala jela mara kadhaa na watoto wangu wanateseka.

April 2012 nikaamua kwenda kanisani kwa mara ya kwanza na baada ya ibada nikamfuata mhubiri na nikamweleza shida zangu na nikaomba usaidizi.