King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

74c3YTe8PYKing-Kaka-has-been-Named-UNICEF-Ambassador-1024x768-1024x768
74c3YTe8PYKing-Kaka-has-been-Named-UNICEF-Ambassador-1024x768-1024x768
Msanii na rapa mkubwa Afrika mashariki King Kaka amefunguka sana kuhusu kufanya muziki na aliyekuwa mpenzi wake Sage.

Katika mahojiano na mtangazaji Rais Papa katika kipindi kinachoruka katika mtandao wa youtube ya Redio Jambo, mkali huyu ameweza kusema kuwa hana matatizo na mzazi mwenzake baada ya wao kutengana huku akisema nafasi ikitokea wanaweza ingia studio na kufanya ngoma.

“Tukikutana studio tunaweza fanya ngoma. Muziki inafanywa tu si ni muziki.” Alisema King Kaka.

Soma mengine:

Papa Na Mastaa ni kipindi na ambacho kimetengwa kwa mahojiano ya kipekee na mastaa wa muziki, mkali huyu ambaye ni mjasiriamali, rapa na mwimbaji pia ameanzisha juhudi za kuwasaidia wasanii chipukizi inayofahamika kama Empires Gold na tayari wasanii watatu wapo katika mpango huo.

King Kaka pia ameweza kuweka wazi sababu iliyomfanya yeye kuacha kufunza masomo ya biashara katika chuo kikuu cha Zetech. Staa huyu aliweka pembeni kazi hii kwa misingi ya kazi nyingi zinazomwandama.

“Nilikuwa mhadhiri Zetech University. Nilikuwa nafunza business na kwa vile schedule yangu ilikuwa tight nkaacha. For almost 2 years sifunzi.”

Mkali huyu aliweza pia kuzungumzia safari yake ya Marekani inayofahamika kama Eastlando Royalty US Tour. Ziara hii ya marekani iliweza kumfanya aingie studio na kumshirikisha msanii wa kimataifa Cassidy katika nyimbo inayofanya vyema ya Far Away.

"The fact that nikona Cassidy kwa ngoma ni ushindi ukubwa," King Kaka alieleza katika kikao cha Papa Na Mastaa.

Pata uhondo hapa:

Audio ya nyimbo hii ilifanywa hapa nchini na Musyoka na video ikihaririwa na mkenya anayeishi Marekani, Hussein Njoroge.

King Kaka alifunguka zaidi kuhusu mahusiano yake na msanii Sage na jinsi anavyotenga wakati kuongea na watoto.

"I think you're talking about sage yeye akona my other daughter. Lazima niende kumwona mtoto wangu ambaye ni Ayana lakini naishi na Nana. You’ve to create time for your kid."

King Kaka hali kadhalika alisema kuwa yupo freshi na Msanii Khaligraph na kumsifia sana.

"Ni jamaa anafanya vizuri tunashukuru mungu. Tukiona vijana wanatia bidii tunafurahia. Anatia bidii kwa kazi zake. Tunaongeaongea ikifika time tutaingia studio."

Soma hapa: