Ilikuaje: Rafiki yangu alinipangia njama nikabakwa - Pauline Juma

Leo katika kipindi cha Bustani la Massawe kitengo cha Ilikuaje, Massawe Japanni aliangazia watoto wa kike wanaokuzwa katika vitongoji duni.

Mgeni wake Pauline Juma, ambaye alilelewa Kibera, alisimulia jinsi rafikiye wa kike alimpangia njama na akabakwa na vijana wanne, mmoja wao akiwa nduguye yule msichana.

Kulingana na bi Pauline, alinajisiwa mwaka wa 2011, Oktober akiwa na umri mdogo wa 16, mida ya saa nne asubuhi.

Nimelelewa Kibera na maisha yalikuwa kujaribu kwani wazazi waling'ang'ana na masomo na nilipofika 16 maisha yangu yalibadilika niliponajisiwa na vijana wanne.

Aliendelea,

Rafiki niliyemdhamini na ambaye nilikuwa namsaidia, alipata mtoto akiwa mdogo alinisaliti. Alinipangia kisa hicho na nduguye alikuwa mmoja wa wale vijana wanne.

Anadai kuwa alinajisiwa kwa takriban lisali moja, kwani mmoja kimnajisi mwingine alikuwa anampiga huku wengine wakimrushia cheche za matusi.

Wahuni wale walidai kuwa mpango wao ni yeye awache shule, apate mtotot ili arudi nyumbani kama yule rafikiye msaliti.

Nikaenda hospitalini huku nikilia na nikamwambia daktari nataka kutibiwa tu ila sitaki kuripoti ili mamangu asiuliwe. Nilimweleza babangu kwani singemwambia mamangu kwani niliambiwa na wale wahuni kuwa wangemuua.

Baada ya kisa hicho, Pauline ambaye alikuwa anasomea Murang'a na alijaribu kujitia kitanzi mara tatu kwani alikuwa akimuuliza mungu maswali megi.

Mara ya kwanza nilijaribu kunywa kemikali fulani na hapo nikapatikana, mara ya pili nilijaribu kutumia kamba kwa chumba cha malazi na mwalimu akanipata.

Mara ya tatu nilijaribu kujigongesha gari katika barabara ya Haile Selassie lakini halikufanyika.

Hapo alifukuzwa shuleni kwani wakuu wa shule hawakutaka jina la shule liharibiwe.

Alitafuta shule nyingine huko Ukambani na hapo ndipo maisha yake yalibadilika na akapata nguvu ya kuendelea na maisha. Hata hivyo kuna wanafunzi ambao walianza uvumi kuwa aliavya mimba na ndio maana alifukuzwa shuleni.

Isitoshe, humo shuleni kuna walimu ambao walikuwa wanampangia njama ili wambake na mmoja wao ilikuwa naibu wa mwalimu mkuu.

Pauline ambaye ana watoto wawili, alipata mtoto akiwa na miaka 19, baada ya kumaliza kidato cha nne baada ya kuanzisha uhusiano na jamaa ambaye aligeuka kuwa mnyama.

Yule jamaa alikuwa ananipiga huku akinikumbusha chenye kilinitendekea na hapo nikaanzisha foundation ya kusaidia wanadada ambao wamepitia mambo kama hayo.

Foundation inaitwa Eagles modelling foundation