'Mimi sio mke wa jamii!' Mwanasiasa Daisy Nyongesa awakanya shemeji zake

daisy nyongesa
daisy nyongesa
Aliyekuwa seneta wa ODM, mheshimiwa Daisy Nyongesa amewasuta shemji zake kwa kile alichokiita kuingilia ndoa yake.

Nyongesa ambaye anajulikana kwa kutoficha yanayomsumbua moyoni, aliwakumbusha kuwa yeye sio mke wa jamii kama ilivyo kuwa mazoea enzi za kale.

Huku akiandika aya ndefu katika mtandao wake wa Facebook Nyongesa alionekana mwenye uchungu mwingi kwani aliwakemea shemeji zake akiwakumbusha kuwa sio haki kujaribu kumthibitishia mumewe kuwa alioa mwanamke asiyefaa.

Alisimulia jinsi dada za mumewe walivyo ungana na kuanza kumpangia jinsi atakavyo ishi, mara hao ndio wanasema idadi na pia jinsia ya watoto anaopaswa kupata.

Isitoshe wao hulalamika kuwa anaishi kwa nyumba kubwa lakini hajifungui watoto, mara hajabadilisha jina lake na kuchukua la ukoo aliko olewa huku wakimkashifu kuwa kazi yake ni kula na kujaza choo.

Aliwatambulisha kama T na M akiwaonya kuwa moto utakao wachoma bado unapashwa misuli nchini Ethiopia.

Siku hizi hatupendezi kila mtu katika kijiji ili tuwe na ndoa yenye furaha, kama waume zetu wana furaha nasi basi hakuna kingine chochote ambacho cha jalisha.

Kama Biblia inavyosema, fanyia wengine jinsi unachotaka wakufanyie. Kwa wazi, wewe ndiye unayepoteza katika uwanja huo. Ndiyo sababu bado wewe hushinda kwa wazazi wako ukitoa wito kama anayeongoza sinema za kutisha.

 Ndiyo sababu ndugu yako huja kwako usiku kutatua shida zako na wakwe wako pamoja na masuala ya mume! Aaaah! Aaaah! Aaaah!

Mheshimiwa Nyongesa kisha aliwapa shemeji zake tahadhari kuwa kamwe habanduki katika ndoa yake licha ya vita anavyopokea kutoka kwao.

Kwa wale ambao wanakabiliwa na vitisho vya aina hii kutoka kwa shemeji zao, simama wima na usiwache mwanamke yeyote kwa jina la dada akufunze jinsi ya kushughulikia mume wako.