Jamaa ashtakiwa kwa kujifanya kuwa afisa wa polisi Voi

Court-Gavel-Thumb
Court-Gavel-Thumb

Mwanamume mmoja alifikishwa katika mahakama ya Voi kaunti ya Taita Taveta hapo jana kwa kujifanya afisa wa polisi.

Reuben Gachanja Kang’ethe alifikishwa mbele ya hakimu Anne Karemi ambapo alikana shtaka hilo.

Mahakama imeelezwa kwamba tarehe 26/5/2019 jamaa huyo alijifanya afisa wa polisi na kuanza kuchukua hongo kutoka kwa waendesha bodaboda mjini Voi  na pia akajaribu kumkamata na kumfunga mfanyibiashara mmoja mjini humo.

Hakimu alimuachilia kwa dhamana ya shilingi laki tatu na mdhamini wa kiwango sawa na hicho au pesa taslimu shilingi laki mbili.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 24 mwezi huu huku ikitarajiwa kusikilizwa tarehe 1 Julai.