Tutaivuruga harusi ya Waiguru! Wauguzi Kirinyaga waapa

Wauguzi katika kaunti ya Kirinyaga wameghadhabishwa na kile wanachokitaja kama utepetevu wa kazi baada ya Gavana Waiguru kutosikiliza kilio chao na badala yake kutishia kuwafuta kazi. Wauguzi hawa walianza mgomo wao siku chache zilizopita na kulemaza huduma katika hospitali kaunti hiyo.

Soma hapa:

Gavana Waiguru ametishia kuwapiga kalamu wafanyakazi hao huku akisema kuwa hataruhusu watu wachache kulemaza shughuli za matibabu Kirinyaga.

"Hatuwezi kukubali watu wa Kirinyaga waendelee kupata tabu kwa sababu ya watu ambao wana ubinafsi wa ajenda zao za kisiasa." alisema Waiguru.

Pata uhondo kamili:

Wauguzi hawa sasa wanatishia kuivuruga harusi hiyo iliyoratibiwa tarehe 13 Julai kati yake na mpenzi wake mwanasheria Kamotho Waiganjo. Sherehe hizi zitafanyika katika shule ya msingi ya Kiamugumo katika kaunti ya Kirinyaga hatua chache kutoka nyumbani kwa gavana huyu.

"Nishamueleza mwanakandarasi anayehusika katika kuiboresha barabara ya Kianyaga- Kiamugumo- Kithure amalizie kazi hiyo kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kwa sababu natarajia wageni." Alisema Waiguru.