Iwapo unataka raha katika ndoa, fuata ushauri wa mke wako - Bahati

Mwimbaji wa nyimbo za injili Kevin Bahati ametoa ushauri kwa wanaume wenzake kuhusu ndoa.

Amewaambia wanaume kuwa wanafaa kuwaruhusu wake zao kuwashauri na watilie maanani ushauri huo iwapo wanataka kuishi maisha mazuri katika ndoa.

Akizungumza wakati wa mahojiano katika runinga ya NTV Bahati alisema kuwa nyumba hulindwa na mke na kuongeza kuwa wanafaa kuwachwa wafanye wanavyotaka pamoja na kuwaelekeza waume zao.

''You know women are the ones who run our homes. Whatever they say should go. By the way, advise to men out there, dear men, if you want to survive, if you want to be happy like me and not stressed like Samir, please allow your wife to hen-peck you. That way, your marriage will be happy," alisema

Alisema haya alipokuwa ajibu swali aliloulizwa, iwapo mke wake amemteka fikra  kwa usemi maarufu hapa kenya iwapo mke  wake 'amemkalia chapati ' . Hata hivyo hii sio mara ya kwanza Bahati ameulizwa swali hili  ikizingatiwa kwamba mke wake amemzidi umri kwa miaka mitatu.

Ni kisa cha hivi majuzi kilichochangia wengi kuamini kwamba Bahati ametekwa fikra, baada ya mke wake Diana Marua kumnyoa nywele zake bila hiari.

Kwangu mimi binafsi nashikilia dhana kwamba ni mwanaume anayefaa kuingoza ndoa na mwanamke amheshimu mume wake. Mwanamke kutoa masharti yote nyumbani ni ishara kuwa hana heshima kwa mumewe.