Cristiano Ronaldo amkaribisha mtoto Klabuni Juventus

66441408_2526528134044284_5693386043142477961_n (1)
66441408_2526528134044284_5693386043142477961_n (1)
Cristiano Ronaldo alimruhusu mvulana mdogo ambaye ni shabiki wake kukaa pamoja naye na timu yake ya Juventus wakati wa Kombe la Mabingwa ya Kimataifa dhidi ya Tottenham siku ya Jumapili.

Erik Lamela alitia Spurs kifua mbili kunako dakika ya 30 kabla ya Gonzalo Higuani akiisawazishia Juventus kunako dakika ya 53. Cristiano Ronaldo alitwapa Juventus uongozi kunako dakika ya 60.
Cristiano Ronaldo alibadilishwa dakika tatu baada ya kufunga bao.
Hata hivyo, alionekana mwenye furaha baadaye kukaa pamoja na Leonardo Bonucci na hapo ndipo shabiki wake, alichukua fursa na kukimbia na kumsalimia Ronaldo.

Ronaldo alimsalimia mvulana huyo kisha wakawa na mjadala mdogo na kisha kumkaribisha kukaa mbele yake na wachezaji wenzake na kuendelea kuuona mchezo ulioendelea.

Mtoto huyo alikuwa na furaha alipoketi pale na kuuona mchezo ulioendela.
Soma mengi

https://twitter.com/SportingLifeFC/status/1152934353250504714