Mwanamuziki maarufu nchini Uganda afariki baada ya kutekwa nyara, kuteswa

ziggy wine
ziggy wine

Mwanamuziki wa kiganda, Allinda Michael ameiaga dunia kufuatia majeraha aliyopata baada ya kutekwa nyara mnamo tarehe 21 mwezi julai. Michael anayetabulika kama Ziggy Wine anasemekana alitekwa nyara na majambazi akiwa safarini kurekodi muziki wake.

Ziggy wine alikuwa mmoja wa wanamuziki kwenye lebo yake Bobi wine huku pia akiwa shabiki mkubwa wake Bobi Wine. Kifo chake kimekuwa pigo kubwa ila Bobi wine anasema kuwa jambo hilo haliwaogopeshi kwani watazidi kutafta uhuru wa taifa lao.

Baada ya kupotea, Ziggy alipatikana wiki moja iliyopita msituni huku akiwa na majeraha kwenye jicho lake moja pamoja na kukatwa vidole viwili. Hata hivyo, familia yake Ziggy inasemekana kukataa kusaidia katika uchunguzi kwani inahofia kuwa huenda maisha yao yakawa mashakani.

Ziggy wine alikuwa shabiki wake Bobi wine pamoja na muungano wake wa 'peoples power ' unao mkashifu rais wa Uganda kwa matendo yake ya kinyama.

Baada ya kuuona mwili wa marehemu Ziggy, Bobi Wine aliwaongoza waganda wengi katika kumuomboleza mmoja wao.