UTAFITI: Mamia hukimbilia bangi ya matibabu kliniki

Mamia ya watu nchini Uingereza sasa wanaelekea katika kliniki za kibinafsi kwa ajili ya kupata dawa za bangi.

Kulingana na BBC, tangu madai hayo kutolewa Novemba 2018, kumekuwa na maagizo machache ya daktari kwa ajili ya dawa ya bangi yenye viungo vya THC na NHS.

Na hii imewafanya baadhi ya wagonjwa wenye magonjwa kama vile kifafa kulipa takriban pauni £800 kila mwezi katika hospitali za kibinafsi.

Serikali inasema inazihurumia familia "zinazokabiliana na changamoto ya magonjwa hayo ".

Cheryl Keen amekuwa akijaribu kupata bangi katika kliniki za serikali kwa ajili ya binti yake Charlotte - ambaye ubongo wake umeharibika na ana ugonjwa wa kifafa - lakini maombi yake yamekataliwa mara mbili .

Na amekuwa akiambiwa kuwa dawa hiyo ni ghali mmo na bado hajatumia dawa nyingine zilizopo, anasema.

"Hakuna kilichotokea , hakuna mabadiliko tangu bangi ilipokubalika kisheria ," Bi Keen ameiambia BBC

"Inakera kabisa kwamba mtu yeyote analazimika kulipia kwenda katika hospitali za kibinafsi ," aliongeza - jambo ambalo anasema hawezi kumudu kulifanya.

Makundi yanayopigania matumizi ya bangi kama dawa katika hospitali za umma yanasema hospitali hizo zinaweka ukomo wa matibabu ya bangi kwa wagonjwa.

Tathmini iliyotolewa mwezi huu , ilionyesha ukosefu wa ushahidi kuhusu usalama wa matumizi ya muda mrefu ya bangi. Na hii imesababisha dawa hizo kuanza kutumiw akatika kliniki za kibinafsi.

Kampuni ya Grow Biotech, inayoshughulia utoaji wa robo tatu ya dawa za mmea wa bangi inayonunuliwa nje ya Uingereza, imesema kuwa kufikia mwezi Julai ilipokea zaidi ya maombi 100 ya maagizao ya madaktari wa kliniki za kibinafsi ambapo 60 kati ya maombi hayo yalitekelezwa.

Tawi jipya la kliniki ya utoaji wa dawa za bangi bado halijafunguliwa lakini linasema kuwa limekwishapokea maombi ya wagonjwa 162 wanaosubiri kupewa awa hizo - wenye magonjwa kama vile kifafa - ulemavu wa ubongo Parkinson's, dawa za baada ya mfadhaiko wa akili miongoni mwa magonjwa mengine.

-BBC