Patanisho: Mwanangu hajaniongelesha kwa mwaka mzima sasa

Mama Caren,47,  ameomba apatanishwe na Kifungua mimba wake winnie, 26, ambaye alitoka nyumbani  mwaka uliopita na hajarudi kwa mwaka mmoja sasa huku pia akiwa amekatisha mawasiliano na mamaye mzazi.

"Mimi ni mama mjane na nimewalea wanangu kwa usaidizi wa baba yao wa kambo. Mwaka uliopita nilimwambia Winnie aniombee shillingi elfu nne ambazo nilikuwa nazihitaji kwa dharura. Hata hivyo, sikuweza kuzipata na kumrudishia na sasa naona hio ndio sababu winnie hajawahi rudi nyumbani tangu mwaka uliopita na amekuwa haniongeleshi hata nikimpigia simu hachukui."

 Winnie ambaye anaishi hapa mjini Nairobi  hata hivyo amemweleza mamake kuwa hajamsahau wala kumkasirikia ila ni matatizo madogo madogo ya kimaisha.

"Mum mimi sina ubaya wowote na wewe. Kukataa kuja nyumbani ni juu leave yangu ilisongeshwa kutoka mwezi wa nane hadi mwezi wa kumi na moja mwaka huu na itakapofika mimi basi nitakuja nyumbani kukusalimia. Mimi Nakupenda sana na pesa haiwezi kunifanya nisikuongeleshe kwa wakati wowote maishani mwangu."

"Mum simu yangu ilibiwa hivo nimekuwa mteja mara nyingi na nimenunua laini nyingine hivi juzi kwa ajili ya mawasiliano. Nitapanga ukuje huku kunitembelea."

Mamake winnie na winnie wamepatanishwa huku Gidi akimwodolea Mama huyo wasiwasi aliokuwa nao moyoni mwake .

"Mimi nakupenda sana mwanangu na ujue nilikuwa na huzuni moyoni mwangu ila sasa hivi nimeridhika."

Gidi amemshauri Winnie awe akimpigia simu mamaye kila wakati ili kumjulia hali na kumpa amani ya moyo wake hasa ikizingatiwa kuwa yeye ni mtoto wa kwanza ndani ya familia hio.